MKUU WA MKOA WA MBEYA AONYA WATAALAMU WA KILIMO
MKUU
wa Mkoa wa Mbeya Bw.Abbas Kandoro amewaonya wataalamu wa kilimo kuacha
kufanya kazi kwa mazoea kwa kukaa maofisini badala ya kwenda mashambani
waliko wakulima na ili waweze kusaidiana wakulima kujua mbinu za bora za
kuboresha mazao yao kuliko kuendelea kufanya kazi za kilimo bila
wataalamu kilimo kuwepo .
Mwandishi
wetu Esther Macha anaripoti kutoka Mbeya kuwa Bw. Kandsoro alisema
wataalamu wa kilimo wanapaswa kuwa karibu na wakulima wao waliopo
vijijini kuliko mazoea yaliyojengeka miongonbi mwao yao ya kukaa
maofisini kusubiri taarifa za kilimo wakati taaluma yao inawataka kufika
mashambani waliko wakulima wenyewe.
Mkuu
huyo wa Mkoa aliyasema hayo baada ya kupewa taarifa ya idara ya kilimo
ya halmashauri ya wilaya ya Mbeya alipofanya ziara na ndipo akakutana na
madudu kama aliyosikia kwenye tarifa ya wilaya ya Mbozi na kuikataa.
Alisema
hatua iliyopo kwa wataalamu kutokuwa karibu na wakulima ndiyo chanzo
kikubwa cha wachuuzi kupata fursa ya kwenda majumbani kwa wakulima na
kununua mazo kisha wanaondoka nayo pasipo hata kulipa ushuru.
Bw.
Kandoro alisema madudu hayo ni pamoja na kuwepo kwa takwimu
zinazoonyesha taarifa za makadirio ya mavuno ya nafaka hali iliyoashiria
mavuno bado yanaendelea ama hayajafanyika wakati umekwisha hivyo
kulipaswa kuwepo takwimu sahihi na si matarajio tena.
“Ndugu
zangu hatuwezi kwenda katika utaratibu kama huu haiwezekani
kabisa.Unasema shughuli zinaendelea! Wapi wanaendelea kuvuna mpaka leo
hii?.Hivi unajua tayari tuko katika msimu mwingine wa kilimo?” alihoji
Bw.Kandoro.
“Kwa
nini mnafanya kazi ya kukokotoa takwimu mkiwa maofisini?Na hili
nimeliona mahala pengi eneo la kilimo lin a ubabaishaji
mkubwa.Mabwanashamba wapo lakini kila kukicha wanacheza na takwimu
maofisini.Vijijini waliko wakulima hawaonekani”
Alisisitiza
kuwa utaratibu maalumu wa ukusanyaji takwimu zinazohusiana na kilimo
ikiwemo kupeleka maaofisa takwimu katika magulio ili waweze kujua ni
kiasi gani cha mazao kinauzwa.
EmoticonEmoticon