KIKUNDI
cha huduma za majumbani Mkoani Mbeya (KIHUMBE) kimesema kuwa bado kina
changamoto kubwa kutoka kwa jamii wakati wa kutoa huduma hizo ambapo
baadhi ya familia pale zinapopewa misaada huuza na wazazi wengine
kudanganya kuwa watoto wao ni yatima ili wapatiwe misaada.
Mwandishi
wetu Esther Macha anaripoti kutoka Mbeya kuwa akizungumza na mtandao
huu ofisini kwake Meneja wa shirika hilo Bw. Bw.Ptolemy Samweli
alisema kuwa kati ya vitu ambavyo vinawapa wakati mgumu katika shirika
hiloi ni pamoja na changamoto hizo za kutoonyesha uaminifu wakati wa
utoaji wa misaada.
“Sisi
tunalenga zaidi watoto yatima lakini kitendo cha wazazi kuongea uongo
ni kitu kibaya sana wakati kuna familia ni maskini kabisa kwanini
sisisaidiwe kwanza hizo,hawa wanaokuja kudanganya unakuta wazazi wao
wapo na wanaokuja kusema ni wazazi wenyewe kuwa watoto hao ni yatima
,tunaomba wazazi wawe na huruma kwani hata hawa walio yatima
hawakupenda”alisema.
Alisema
kuwa wangependa kusaidia na jamii zingine lakini lengo ni kusaidia
kwanza yatima ambao hauna mwelekeo wowote wa kimaisha, na fedha
wanazopewa ni kidogo na wadhadhili ambazo zimelengwa kwa watu maalumu
tu.
Akizungumzia
kuhusu magodoro ambayo wamekuwa wakipewa na shirika hilo Bw. Samweli
alisema kuwa baadhi ya familia zimekuwa zikidiriki kuuza ili waweze
kupata fedha kitu ambacho si kizuri.
“Si
jambo jema kwani mtu unapopewa msaada ili ukusaidia hutakiwi kuuza,
hata kama una matatizo yako basi tafuta nyingine ya kutatua lakini si
kuuza kwani kama shirika tunapojaribu kutoa misaada hiyo kwa jamii hizi
tunaweka usawa Fulani wa maisha kwao”alisema Meneja huyo.
Aidha
Meneja huyo alisema wagonjwa wengine kuacha dawa na kuipa hasara
serikali na kwamba kwani baada ya kuacha ugonjwa huo hurudi kwa kasi
kubwa.
Akizungumzia
jinsi ya kuwatambua watoto yatima Bw.Samweli alisema katika halmashauri
ya Jiji la Mbeya kuna program maalumu ya ya kuwatambua watoto yatima
ambayo ipo Ustawi wa Jamii ambapo wao kama shirika hufika na kuwachukua
hapo ambao tayari wanakuwa wamehakikiwa na serikali ya Mkoa.
Alisema
katika kufanya hivyo ndo wanakuwa wamepata uhakika kuwa wamepata
watoto hao licha ya kuwa bado kunakuwa na mahitaji makubwa ya watoto
kuhitaji kuhudumiwa na shirika,lakini bado uwezo mdogo kama watoto
wanachukuliwa inabidi wapewe huduma zote kulingana na mahitaji.
EmoticonEmoticon