Mmoja kati ya washiriki wa shindano hilo akionyesha uwezo wake katika kuonyesha kipaji chake
Jitihada za mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) katika kuhamasisha michezo mbali mbali kwa vijana wa jimbo la Iringa mjini zimeendelea kuzaa matunda baada ya leo kutekeleza ahadi yake ya kuanzisha mashindano ya kuibua vipaji kwa wasanii hao.
Baadhi ya washiriki na watazamaji wa shindano hilo wakiwa ukumbini leo
Jitihada za mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) katika kuhamasisha michezo mbali mbali kwa vijana wa jimbo la Iringa mjini zimeendelea kuzaa matunda baada ya leo kutekeleza ahadi yake ya kuanzisha mashindano ya kuibua vipaji kwa wasanii hao.
Katika shindano hilo la kutafuta vipaji kwa awamu ya kwanza katika mkoa
wa Iringa limeonyesha kuwa na mvuto mkubwa kwa wakazi wa Manispaa ya
Iringa ambao wamejitokeza kwa wingi ukilinganisha na makisio ya kuwa
na washiriki wachache zaidi .
Shindano hilo la Kabati katiba star search limefanyika kwa mafanikio
kwa vijana wengi wenye vipaji kujitokeza na kuonyesha vipaji vyao katika
ukumbi wa hallfear mjini Iringa.
Katika shindano hilo wasanii wengi vijana waliweza kuimba mbela ya
majaji Eddo Bashir(Ebony Fm) Temmy Mahondo wa radio country fm, dj Ammy
Yeyo( Country fm )Agnes Anderson(ebony Fm na Dj Muba wa radio Ebony
Fm huku majaji hao wakionyesha kutoamini kutokana na umahiri wa
wasanii hao.
EmoticonEmoticon