Mwanasiasa mwenye utata wa Afrika
Kusini Julius Malema amefikishwa
mahakamani akikabiliwa na shtaka la kuhaulisha pesa au
kujipatia pesa haramu, huku mamia ya wafuasi wake
wakikusanyika nje ya mahakama kumuunga mkono.
Ingawa mahakama ilimwachilia
kwa
dhamana ya randi elfu kumi.
Seng'enge zilizungushwa katika eneo la mahakama hiyo
iliyopo Polokwane, mji mkubwa wa jimbo
analotokea mwanasiasa
huyo,Limpopo.
Malema pia anatuhumiwa kwa kutumia
vibaya
wadhifa aliokuwa nao kama
mkuu wa
chama tawala cha African National
Congress (ANC) tawi la vijana.
Wafuasi wake wanasema
mashtaka hayo yameshinikizwa kisiasa.
Wakiimba na kucheza nje ya mahakama
hiyo
wafuasi wengi wa chama hicho cha ANC tawi la
vijana walishikilia mabango yaliosema
'Muacheni kiongozi wetu'.
Kuna maafisa wengi wa usalama
lakini hali ni tulivu.
Julius Malema na
washirika wake wa kibiashara
wanashutumiwa kwa kufaidi kutokanana na mikataba ya
serikali katika jimbo la
Limpopo, tuhuma ambazo anazikana. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka
31 pia anachunguzwa katika kesi tofauti ya ukwepaji
kulipa ushuru.
Malema ni maarufu sana
Afrika kusini kwa ukakamavu wake wa kutetea
maslahi ya
wananchi na maisha yake ya kifahari, huku akijitambulisha kama mpiganiaji
uhuru wa
uchumi.
Alitimuliwa kwenye
chama hicho tawala mnamo mwezi Aprili
akishutumiwa
kwa
kuzusha migawanyiko katika chama
hicho.
Ni mkosoaji mkali wa a Jacob
Zuma, hivi karibuni akimshutumu rais huyo kwa
alivyoushughulikia mgomo wa wachimba migodi wa
Marikana.
Kwa mujibu wa mwandishi wa
masuala ya Afrika, Andrew
Harding, baadhi ya watu Afrika kusini wanaamini
anafikishwa
haraka mahakamani, ikiwa ni chini ya wiki moja baada ya
kutolewa
waranti ya kukamatwa kwake, ili
kuimarisha nafasi ya kisiasa ya Zuma.
EmoticonEmoticon