Muungano wa Ulaya umeamua kusitisha msaada
kwa
Rwanda.
Uamuzi wa Muungano huo umefikiwa kufuatia
ripoti ya baraza la usalama la Umoja huo iliyodai kwamba
Rwanda inaunga mkono waasi wa M23
dhidi ya serikali ya Congo.
Waasi hao
wanadhibiti kimabavu sehemu kubwa ya Mashariki mwa Jamuhuri
ya Kidemokrasia ya Congo na hata kuwatoza kodi
wananchi.
Kundi hilo lilianza uasi katika eneo hilo mwezi Aprili na kusababisha
takriban
watu nusu milioni kukimbilia usalama wao.
Lakini Rwanda imeendelea kukana madai
hayo.
Umoja wa Mataifa unafanya mkutano na
baadhi ya yatakayopewa kipaombele kwenye mkutano huo ni
swala
la mgogoro huo Mashariki mwa Congo.
Mapema mwezi Julai Marekani ilizuia dola 200,000 zilizokusudiwa
kulisaidia jeshi la Rwanda.
Msaada wenyewe uliokatwa siyo mkubwa kwa jeshi la
Rwanda, lakini hatua hiyo ilitoa
ishara kubwa.
EmoticonEmoticon