Rais Omar Al Bashir wa Sudan na mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir , wamekuwa wakifanya majadiliano mjini Addis Ababa tangu Jumapili.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Sudan, El Obeid Al Morawah amesema, Jumanne katika siku ya tatu ya mazungmzo nchi hizo mbili zilikubaliana . lakini anasema bado kuna vizuizi kuhusiana na suala la mzozo wa kumiliki eneo la Abyei lenye utajiri wa mafuta.
Nchi hizo pia zinajadili kubuni eneo lisilokuwa na shughuli za kijeshi kwenye mpaka wao, eneo la kilomita 23. Lakini suala hilo pia bado linabaki kuwa suala gumu.
Mkutano baina ya marais hao wawili uliopangwa kufanyika Jumanne asubuhi uliahirishwa hadi jioni. Msemaji Al Morawah anasema ikiwa nchi hizo mbili za Sudan zinaweza kukubaliana juu ya Abyei na eneo la kilomita 23, basi masuala mengine yalosalia yanaweza kutatuliwa vilevile.
EmoticonEmoticon