Waandihsi wa habari wakifuatilia kwa makin maelezo toka kwa Mkurungezi wa mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti John Wanyancha mapema leo katika kiwanda cha SBL Mwanza. |
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha,akiongoza waandishi wa habari kutembelea baadhi ya maeneo ya kiwanda cha SBL Mwanza. |
Meneja wa upishi wa bia wa Kiwanda cha Serengeti Rolinda Samson(Brewing Manager) akitoa ufafanuzi wa jambo jinsi utengenezaji wa bia unavyofanyika kwa waandishi wa habari jijini Mwanza mapema leo. |
Mwanza, Septemba 07, 2016 - Hamasa inayotokana na mradi wa kilimo biashara wa kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa kuwawezesha wakulima wa mahindi, mtama na shayiri katika maeneo mbalimbali nchini imewezesha kampuni hiyo ya bia kuongeza kiwango cha malighafi inayotumika kutoka ndani ya nchi kufikia tano 10,000 sawa na asilimia 60 ya malighafi yote inayotumia kuzalisha bia kwa mwaka.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika kiwanda cha SBL Mwanza leo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, John Wanyancha alisema aina sita za bia zinazozalishwa na kampuni hiyo zina asilimia 100 ya malighafi inayoizalishwa ndani ikiwa ni matokeo ya mradi wa kilimo biashara ambao ulianza miaka mitatu iliyopita.
Aina hizo za bia ni pamoja na Pilsner, Kibo Gold, Kick, Uhuru na Senator Lager. Kwa mujibu wa Wanyancha bia mbili za Pilsner na Kibo Gold zimeshinda tuzo za kimataifa mwaka huu ikiwa ni kielelezo cha ubora wa hali ya juu wa bidhaa hizo..
Kupitia programu hiyo kampuni ya Bia ya Serengeti inatoa mbegu zilizo na ubora kwa wakulima bure, kuwaunganisha na taasisi za kifedha ili kupata mitaji inayohitajika kwa ajili ya kilimo cha mashamba makubwa hali kadhalika kuwaunganisha na wasambazi wa mbolea na dhana nyninginezo za kilimo. Kwa upande wake SBL imekuwa ikinunua mazao yote kutoka kwa wakulima hawa na hivyo kuwawezesha kulipa mikopo ya mitaji pamoja na kuboresha hali zao za kiuchumi.
“Hadi sasa mradi huu umeshawanufaisha wakulima zaidi ya 100 kutoka mikoa kadhaa ikiwemo Arusha, Manyara, Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Morogoro, Shinyanga na Dododoma ambao kwa pamoja wanalima takribani ekari 20,000,” alisema mkurugenzi huyo.
Wanyancha alisema kwamba kampuni hiyo imepanga kuendelea kupanua programu hiyo ili kuwafikia wakulima wengi zaidi ili kufikia lengo la kuongeza upatikanaji wa malighafi kutoka ndani hadi asilimia 80 kwa mwaka huu. Mbali na manufaa mbalimbali ya kichumi kwa wakulima, bali zitokanazo na malighafi zinazozalishwa nchini ni za bei nafuu ikilinganishwa na zile zinazotengeneza na malighafi kutoka nje ya nchi.
Mwisho
EmoticonEmoticon