Hii ni Nyumba mpya atakayohamia Rais Barack Obama baada ya kuondoka White House


Rais wa Marekani Barack Obama atapanga nyumba Washington, D.C baada ya kuondoka katika Ikulu ya Marekani (White House) hapo mwakani ambapo rais mwingine wa taifa hilo ataapa kushika madaraka baada ya Barack Obama kumaliza mihula yake miwili ya uongozi.
Nyumba hiyo ilijengwa mwaka 1928, ina vyumba 9 vya kulala, vyumba 8 vya kuogea. Nyumba hiyo yenye muonekano wa kuvutia iliuzwa zaidi ya dola milioni 5 (TZS bilioni 10.9) mwaka 2014.
Rais Obama amesema kuwa yeye na familia yake watabaki Washington baada ya kutoka Ikulu ya Marekani (White House) Januari 2017.
“Tutaendelea kuishi in Washington D.C. hadi hapo Sasha (Binti yake mdogo) atakapohitimu sababu kumhamisha mwanafunzi shule katikati ya muhula ni ngumu” alisema Rais Obama.
Hizi hapa chini ni picha za nyumba atakayoishi Rais Obama atakapotoka madarakani.
160525142925-obamas-house-1-exlarge-169 160525143007-obamas-house-2-exlarge-169 160525143029-obamas-house-3-exlarge-169 160525143046-obamas-house-4-exlarge-169 160525143107-obamas-house-5-exlarge-169 160525143129-obamas-house-6-exlarge-169 160525143149-obama-house-7-exlarge-169 160525143218-obama-house-9-exlarge-169 160525143238-obama-house-10-exlarge-169 160525143256-obama-house-11-exlarge-169 160525143312-obama-house-12-exlarge-169 160525143327-obama-house-13-exlarge-169 160525143536-obama-house-14-exlarge-169 160525143605-obama-house-15-exlarge-169 160525144122-obama-house-16-exlarge-169
Previous
Next Post »