Kimazingira Tanzania, ni moja ya nchi ambayo
imejaliwa sana hapa duniani kuwa na fursa nyingi za wazi ambazo ukizitumia ni
lazima ufanikiwe. Lakini pamoja na wingi wa fursa hizo ambazo zinaweza kutumiwa
na kuleta mafanikio kwa taifa lakini bado kumekuwa na wimbi kubwa la watu ambao
hawana ajira.
Kutoka
na ukosefu wa ajira vijana wengi
wamekuwa wakihaha kutafuta ajira huku na huko bila matumaini. Ni tatizo
ambalo
limekuwa likisumbua sana si kwa wazazi tu pekee ambao ni wahanga watoto
hao, bali hata taifa kwa ujumla. Lakini yote hayo yamekuwa yakitokea na
kusahau
kwamba tupo kwenye nchi mbayo ina utitiri ama wingi wa fursa za
kutosha.
Kwa
kuwa fursa hizi zipo ni matumaini yetu
kwamba, badala ya vijana wetu hawa waliomaliza vyuo vikuu kukimbilia
ajira
ambazo tena kwa sasa ni finyu, ni vyema wakazitumia fursa
zinazowazunguka
kuwafanikisha. Kwa kusoma makala haya, utajifunza fursa ambazo zinaweza
kumsaidia kijana wa kitanzania popote alipo kujiajiri na kutengeneza
mafanikio makubwa kuliko kubweteka peke yake kwa kusubiri ajira.
1.
Kilimo cha kisasa kwa kutumia hema.
Hiki ni kilimo kigeni kwa wengi ambacho
kinatumia teknolojia ya kisasa ya hema. Lakini pamoja na ugeni wake hiki ni
kilimo ambacho pia kinaweza kutatua tatizo la ajira kwa uhakika. Kwa nini iko
hivyo? Hiyo ni kwa sababu pato lake linakuwa kubwa na la uhakika ingawa eneo la
kulima linakuwa dogo.
Kwa kutumia kilimo hiki kijana anaweza
kuchangamkia fursa hii na kuajiri. Hapa kijana
anaweza kujiajiri kwa kujihusisha na kilimo hiki kuliko kukaa na kutegemea
ajira peke yake. Kwa mfano, wataalamu wanatuambia katika eneo dogo lenye urefu
wa mita kumi na tano na upana wa mita nane lina uwezo wa kutoa tani za nyanya
zisizopungua kumi ikiwa litasimamiwa vizuri kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kwa hiyo utaona kwamba kwa kijana ambaye yupo
makini na ameamua kuwekeza akitoa nguvu zake nyingi kujihusisha na kilimo hiki
basi atakuwa yupo sahihi kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine. Kitu kikubwa
cha kuzingatia ni kuwa tayari kutoa
gharama zinazohusika hadi kilimo hiki kikafanikiwa na kuwa chenye manufaa
makubwa kwa kila kijana mwenye uthubutu.
MKOMBOZI KWA MKULIMA |
2.
Ufugaji wa nyuki.
Kati ya miradi ambayo naweza kusema ni rahisi
kwa kijana yeyote yule wa kitanzania ni ufugaji wa nyuki. Ni moja ya mradi ambao
unaweza ukafanywa katika mazingira tuliyonayo bila kuhusisha gharama kubwa sana
na ikawa ni chanzo kimojawapo cha kujiajiri na kuingiza kipato kikubwa. Ufugaji huu hauhitaji gharama
kubwa sana mara nyingi unafanywa kulingana na pato alinalo mwenye nia ya
kuwekeza.
Tuchukulie kwa mfano kwa kijana ambaye hana
mtaji anataka kufuga nyuki ili wamzalishie asali hapa anafanyaje? Kitu ambacho
anaweza akafanya si lazima awe na mizinga ya kisasa. Anaweza akatengeneza
vibuyu au magome ya miti na kuweka mizinga yake kwa ajili ya ufugaji rasmi. Baada
ya kuweka mizinga inatakiwa aweke mazingira rafiki ya kuvutia nyuki kama maji
na nta.
Kwa kijana amabaye atafanikiwa kujihusisha na
ufugaji huu na akasimamia vizuri, ni ushahidi tosha hata hiyo ajira hatoitaka
tena kutokana na pesa atakayoingiza. Hii ni moja ya fursa kubwa sana ambayo inatoa ajira isipokuwa vijana wengi
wanakuwa kama wamefungwa macho kwa kushindwa kuona ni nini cha kufanya na
kujikuta kukimbilia mjini ambako ajira zenyewe zimekuwa ni kwa uchache.
WEKA MIZINGA BORA. |
3. Kilimo cha mazao ya biashara.
Mbali na ufugaji wa nyuki na kilimo cha hema,
kijana anaweza kuchangamkia fursa ya kufanya kilimo cha mazao ya biashara. Mazao
haya yanaweza yakawa kama karanga,
choroko, kunde, alizeti au hata pamba lakini hiyo yote inategemea sana
na eneo ambalo upo urahisi wa kipi kwako cha kufanya.
Kitu kikubwa ni kule kufuta mitazamo hasi
kwamba kilimo ni cha watu duni hiyo siyo kweli. Watu wengi wanaoendesha maisha
yao vizuri sana kwa kutegemea kilimo hiki cha kisasa. Anza kwa kujifunza kwa
wale wakulima waliofanikiwa na kisha changamkia fursa ya kilimo hiki ambacho
kinaweza kikawa mwanzo wa ajira kubwa kwako kuliko unavyofikiri.
Kwa kijana ambaye ataingia kwenye kilimo hiki
kikamilifu na akasimamia masoko vizuri, njia ya mafanikio itaonekana kwake. Uzuri
wa kujihusisha na kilimo hiki cha mazao ya biashara hata soko lake mara nyingi
linakuwa kubwa hali ambaye hupelekea kupata faida kubwa kwa mkulima. Hivyo ni
wito wetu kuhakikisha vijana wengi wanaolia ajira hakuna kulizingatia hili sana na kuamua kuchukua hatua.
IKILIMWA VIZURI, PATO NI KUBWA. |
4. Ufugaji wa samaki.
Pia ufugaji wa samaki unaweza ukawa ni chanzo
kizuri cha kipato kwa vijana wengine ambao hawana kazi hasa katika yale maeneo
ambayo ni shida kupatikana kwa samaki. Ufugaji huu unaweza ukafanywa kwa kuchimba bwawa dogo la samaki
na kuanza kutengeneza pesa. Bwawa si lazima liwe kubwa sana linaweza
likawa dogo hata la mita 'square' mia nne.
Uzuri wa kufuga samaki ni kwamba kwanza wanachukua
muda mfupi, pia inachukua miezi minne kukua. Lakini hiyo haitoshi upatikaji wa
vifaranga wa samaki pia sio mgumu na vinapatikaana kwa bei rahisi. Lakini uzuri
mwingine si kupatikana kwa vifaranga tu,
bali hata pato lake linakuwa ni kubwa kulingana na kile ulichowekeza kwa muda mfupi.
BWAWA LA KUCHIMBWA LA SAMAKI. |
Wataalamu wanatuambia hivi, kwa mfano kama umeweka
samaki kwenye bwawa dogo la mita square mia nne. Kwanza bwawa hilo linauwezo
wakuchukua samaki elfu nne. Sasa kama eneo hilo linachukua samaki hao na kila
samaki akawa na nusu kilogramu, basi kwa bwawa hilo ndani ya miezi minne utapa
milioni nane hata kama kilo moja hapo utauza kwa shilingi elfu nne.
Hizi ni baadhi ya fursa chache ambazo kijana
wa kitanzania anaweza kuzitumia kufanikiwa. Ingawa hata hivyo kijana anaweza
kujihusisha na mambo mengine zaidi ya kumuingizia kipato kama ufugaji wa kuku kwa
kisasa au hata kilimo cha matunda.
Chukua hatua kufikia mafanikio makubwa na acha
kuendelea kulia eti ajira hakuna, yapo mambo mengi ya kufanya.
credit to DIRA YA MAFANIKIO
EmoticonEmoticon