Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto) akitoa
salamu za Serikali kwa Mbwana Samatta kufuatia mafanikio ya ushindi
alioupata katika mchezo wa soka. Serikali ya Tanzania pia imempatia
kiwanja katika eneo la Kigamboni huku hati ya kiwanja hicho akitarajiwa
kukabidhiwa hapo baadae.
Usiku wa
Januari 12, Mbwana Samatta alikuwa na shughuli maalum “Samatta Party.”
kwa ajili ya kusheherekea ushindi wake alioupata wa kunyakua tuzo ya
mchezaji bora wa Afrika anayechezea ndani ya Bara la Afrika. Katika
tukio hilo viongozi mbalimbali wa Serikali na wadau wa soka walikuwapo
ambapo Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh. Lukuvi
alimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Ambapo alimtaka Mbwana Samatta kuendelea kutumia vizuri kipaji chake kwani ni nguzo ya Taifa kwa sasa baada ya ushindi huo.
Mbwana
Samatta akimkabidhi mgeni rasmi katika tukio hilo, Mh. Waziri William
Lukuvi jezi yake aliyokuwa akiitumia katika klabu ya TP. Mazembe ya DRC
Congo.(P.T)
Mshindi
wa Big brother 2014,Idris Sultan akipata picha pamoja na tuzo ya
mchezaji bora wa Afrika anayechezea ndani ya Bara la Afrika Mbwana
Samatta.
Baadhi ya
marafiki wa Mbwana Samatta waliowahi kucheza pamoja enzi za utoto
ikiwemo mpira wa mtaani wakati huo maarufu ‘chandimu’ nao walikuwapo
kumpa pongezi.
Samatta akiwa pamoja na wageni akiwemo waziri Lukuvi, Nape na wazazi wake wakifuatilia shughuli hiyo inavyokwenda.
EmoticonEmoticon