Mmiliki
wa kiwanda cha uongezaji thamani madini ya jasi kilichopo mkoani
Singida, Emmanuel Shilla akimuonesha Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto) moja ya bidhaa za urembo wa
ndani ya nyumba unaotengenezwa kutokana na madini ya jasi yanayopatikana
mkoani Singida.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto)
akitazama jinsi madini ya jasi yanavyotumika kutengeneza vitu mbalimbali
ikiwemo urembo wa ndani ya nyumba mara baada ya kutembelea kiwanda cha
uongezaji thamani madini ya jasi cha Singida Cornice.Aliyevaa shati
jeupe ni mmiliki wa kiwanda, Emmanuel Shilla.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akiangalia
jinsi mtambo wa bayogesi ulivyomwezesha mmiliki wa mtambo huo, Habiba
Sengasu (kulia) kupata faida mbalimbali ikiwemo nishati ya kupikia.
Naibu Waziri aliutembelea mtambo huo akiwa katika ziara ya kukagua
miradi ya Nishati na Madini mkoani Singida.
Mafundi
wakiendelea na ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme kilichopo mkoani
Singida ambacho kinatarajiwa kuanza kazi mwezi Juni mwaka huu. Ujenzi wa
kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa miundombinu ya
usafirishaji umeme wa kilovolti 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga
unaotarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu. Kituo kinajengwa na
kampuni ya GSE&C na Hyosung kutoka Korea.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akizungumza na
wachimbaji wa madini ya jasi mkoani Singida wakati alipofika wilayani
Manyoni mkoani Singida ili kukagua shughuli za uchimbaji wa madini hayo
na kuzungumza na wachimbaji wadogo.Wa kwanza kushoto ni Yusuph Kibira na
katikati ni Ismail Ivata
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kushoto)
akiangalia moja ya mitambo ya bayogesi inayomilikiwa na Habiba Sengasu
(wa kwanza kushoto) mkoani Singida. Naibu Waziri aliutembelea mtambo huo
akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya Nishati na Madini mkoani
Singida.
Na Teresia Mhagama, Singida
Serikali imesema kuwa itanyang’anya vitalu vya madini visivyoendelezwa na kuwapatia wachimbaji wadogo nchini ili waviendeleze.
Hayo
yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani
wakati akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Fatma Toufiq kabla ya
kukagua miradi ya uchimbaji madini pamoja miradi ya umeme wilayani humo.
“Tutachukua
maeneo yasiyoendelezwa na kuwagawia wachimbaji wadogo kama sheria ya
madini ya mwaka 2010 inavyoelekeza hivyo Kamismhna Msaidizi wa Madini
Kanda hii ya kati hakikisha hilo linatekelezwa,’’ alisema Dkt. Kalemani.
Naibu
Waziri alitoa agizo hilo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Fatma
Toufiq kumueleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wachimbaji
wadogo katika wilaya hiyo ikiwemo utumiaji wa zana duni za uchimbaji
madini pamoja na ukosefu wa maeneo ya uchimbaji madini kutokana na watu
wengi kuhodhi maeneo hayo kwa muda mrefu bila kuyafanyia kazi.
Aidha,
Mkuu wa wilaya alimueleza Naibu Waziri kuwa licha ya changamoto za
wachimbaji wadogo, wilaya hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya umeme
kukatika mara kwa mara jambo ambalo linaathiri shughuli za kiuchumi za
wananchi katika wilaya hiyo.
Akifafanua
suala hilo Naibu Waziri alimueleza kuwa umeme katika wilaya hiyo na
mikoa ya Iringa, Singida, Dodoma na Kanda ya Ziwa utatengemaa mara baada
ya ujenzi wa njia kuu ya umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka Iringa
hadi Shinyanga kukamilika mwezi Juni mwaka huu kwani mitambo hiyo
itasafirisha umeme kwa kiwango kikubwa tofauti na miundombinu ya sasa
ambayo inasafirisha umeme kwa msongo kilovolti 220.
Hata
hivyo Naibu Waziri aliwataka watendaji wa Tanesco katika wilaya hiyo
kuhakikisha kwamba umeme haukatiki kwa sababu ya uzembe wa kibinadamu
kufanya au kutokufanya kitu fulani bali utokane na majanga ya kiasili
ambayo hayazuiliki.
“
Watendaji wa Tanesco nileteeni taarifa kwa nini umeme unakatika mara kwa
mara katika wilaya hii na kama ni uzembe wa mtu basi naye akatike
hapohapo,” alisisitiza Dkt. Kalemani.
Wakati
huohuo Naibu Waziri ameitaka kampuni ya spencon iliyopewa tenda ya
kusambaza umeme katika vijiji 90 mkoani Singida kukamilisha kazi hiyo
ifikapo mwezi Mei mwaka huu.
Naibu
Waziri alitoa agizo hilo baada ya kampuni hiyo kusuasua katika kusambaza
umeme vijiini kwani kazi ya kusambaza umeme katika vijiji hivyo
ilipaswa kukamilika mwezi wa 11 mwaka jana lakini hadi sasa wamesambaza
umeme katika vijiji 17 tu.
“Mradi
huu unahusisha kilomita 188 lakini mpaka sasa nguzo zimefikia kilomita
48 tu, asipokamilisha kazi hii kwa muda huu tuliompa tutataifisha mali
zake, na watendaji wa Tanesco mniletee taarifa ya kina sababu za mradi
huu kuchelewa na hatua mlizochukua,” alisema Dkt. Kalemani.
EmoticonEmoticon