Brown alikiri makosa ya kushambulia Rihanna mwaka 2009
Polisi
katika jiji la Las Vegas, Marekani wanachunguza madai kwamba mwanamuziki
mashuhuri wa R&B Chris Brown alimpiga mwanamke Jumamosi.
Mwanamke huyo anadai msanii huyo alimgonga usoni alipojaribu kumpiga picha.
Kisa hicho kinadaiwa kutokea katika hoteli alimokuwa Chris Brown mapema Jumamosi asubuhi.
Mwanamuziki huyo hajazungumza lolote kuhusiana na madai hayo.
Chris Brown na Rihanna walikuwa wapenzi
Mwaka
2009, Brown aliagizwa kukaa miaka mitano bila kufanya kosa baada ya
kupatikana na hatia ya kumpiga nyota wa muziki wa pop Rihanna
EmoticonEmoticon