JAMAA AMEKAA MIAKA 27 GEREZANI, MAHAKAMA IMEGUNDUA ALIFUNGWA KIMAKOSA HAKUWA NA HATIA, IMEAMUA KUMUACHIA HURU NA WATAMLIPA KIASI HIKI.


Jamaa amekaa miaka 27 gerezani, Mahakama imegundua alifungwa kimakosa hakuwa na hatia, imeamua kumuachia huru na watamlipa kiasi hiki.Kwame Ajamu alikuwa na miaka 17 wakati alipopatikana na hatia ya mauaji miaka kadhaa iliyopita.

Bwana huyo mkazi wa Ohio Marekani kwa sasa ana umri wa miaka 57, jumanne iliyopita mahakama ilimfutia mashtaka yake kabisa kudhihirisha kuwa walimuhukumu kimakosa hakuhusika na kesi hiyo.

Unaambiwa jamaa baada ya kutumikia Theluthi ya kifungo chake, mwaka 2003 alipewa Parole na Magereza ( ni utaratibu wa kisheria unaompa fursa mfungwa aliyehukumiwa kutumikia kifungo gerezani cha miaka minne na kuendelea kutumikia sehemu ya kifungo chake katika jamii kwa masharti maalum). Baada ya kupata Parole Kwame akaamua kukata rufaa zaidi ili kutafuta haki yake.

Mahakama inasema alietoa ushahidi dhidi yake alikuwa na maslahi binafsi, Tayari amepoteza miaka 27 gerezani na Serikali imesema itampa kiasi cha shilingi milioni 80 kwa mwaka kama fidia yake.

Previous
Next Post »