Katika siku yake ya kwanza mara baada ya kuapishwa kuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli amefanya ziara ya
kushtukiza kwa kila wizara ambapo ametoka Ikulu kwa kutembea kwa miguu mpaka
wizara ya fedha na kukuta watumishi walio wengi hawapo na kukuta watu wa chache
ndani ya ofisi hizo.
Wakati wa ziara hiyo ambayo alizungukia kila ofisi pasipo
watumishi hao kufahamu Rais.Dk.Magufuli aliingia kila ofisi ambapo akikuta
anayehusika na kazi Fulani hayupo mahala pake anahoji anao wakuta ndani ya
ofisi na hivyo kuondoka na kila mmoja wao kushangaa nini hatua zinazo fuata.
Ziara yake hiyo iliyochukua dakika 10 ya kutembea kwa mguu kutoka ikulu hadi wizara ya fedha imewashangaza wananchi waliowengi ambao wamemuona kutokana na ikiwa ni siku moja kuapwishwa kwake kuwa Rais wa Tanzania kwani hawakuwa na mawazo wangeweza kumuona mkuu huyo wan chi akiwa anatembea kwa miguu kama mwananchi wa kawaida hali ambayo imefanya wananchi waamini kauli mbiu yake wakati wa kampeni ya Hapa Kazi Tu kwamba huenda ndio imeanza.
Hata hivyo Rais.Dk.Magufuli baada ya ziara hiyo ya
kushtukiza inaelezwa kuwa anafanya kikao hivi sasa na wakuu mbali mbali huenda
baada ya kikao hicho kina majibu mazito.
Zoezi hilo amelifanya mara baada ya kumaliza kumuapisha mwanasheria mkuu wa serikali ya awamu ya tano George Masaju Mapema Leo.
Zoezi hilo amelifanya mara baada ya kumaliza kumuapisha mwanasheria mkuu wa serikali ya awamu ya tano George Masaju Mapema Leo.
EmoticonEmoticon