Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo usiku wa October 1 amefanyiwa sherehe Santiago Bernabeu ya kusherehekea rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid, licha ya kuwa Ronaldo inadaiwa yuko sawa kwa magoli na Raul kwa idadi ya magoli 323, lakini gazeti la Spanish na klabu yao inaeleza kuwa Ronaldo ana jumla ya magoli 324.
Shughuli hiyo ilihudhuriwa na wachezaji wenzake wa Real Madrid, Rais wa klabu hiyo Florentino Pérez pamoja na wakala wake Jorge Mendes, licha ya kuwa Cristiano Ronaldo
hakuwa katika mahusiano mazuri na vyombo vya habari toka mwezi March
2015, ameomba radhi kwa vyombo hivyo sambamba na kuwashukuru makocha
waliowahi kumfundisha.
Katika sherehe hiyo Ronaldo alipewa kiatu cha mfungaji bora na Rais wa Real Madrid Florentino Pérez sambamba na mpira wa zawadi. Licha ya kuwa Jose Mourinho aliwahi kuongea kauli ya kejeli dhidi yake Ronaldo amemshukuru kocha huyo pamoja na wachezaji wenzake wa Real Madrid.
EmoticonEmoticon