Vijana Saba wa Jeshi la
kujenga Taifa(JKT) kikosi cha 821 Bulombora wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma waliofariki
katika ajali baada ya gari wallokuwa wakisafiria kupinduka jana huku wengine 22
wakijeruhiwa wametambulika.
Kamanda wa Jeshi la wananchi
mkoa Kigoma, Kanali Mamdadi Kisui alisema kuwa wapiganaji hao walikumbwa na
mauti hayo majira ya saa 10 jioni katika eneo la Mlima Pasua nje kidogo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Kanali Kisui alisema kuwa
wapiganaji hao walikuwa wakisafiri na gari la Jeshi aina ya Iveco lenye namba
za usajili 5717 JW 09 lililokuwa likitokea kambi ya Burombola kuelekea mjini
Kigoma likiwa na jumla ya vijana 30 wa JKT.
Mganga Mfawidhi wa hospitali
ya Mkoa kigoma Maweni,Dk.Fadhili Kibaya aliwataja Askali waliofariki katika
ajali hiyo kuwa Ally Kambagwa Mkazi wa Mtwara, Abeli Maisha Mkazi wa Morogoro,
Eugini Bitati Mkazi wa Kibondo Mkoani Kigoma, Saidi Sadara Mkazi Wa wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga, Bakari Kibaya Mkazi wa Tanga na Fredric Kaemela Mkazi wa Njiro
mkoani Arusha.
Majeruhi wa Ajali hiyo ni:- Benedict Ndokeye, Raphaeli Johanna, Athanasi
Emanuel ,Abui Nzoge, Abubakari Piter, Abubakari Msubi, Deusi Manyanya, Edward
Nyanda, Eliasi Magesa, Geofly Maliki, King Kasefu, Kamiliusi Agida, Lameki John,
Maltini Kupatu, Stevin Denisi, Saidi Omary, Saidi Zuberi, Shabani Zakaria, Victer
Saverxy, Jacksoni Nyarubu, Muhamed Nyimbo.
Miili ya marehemu imeagwa leo
katika hospitali ya mkoa Kigoma na baadaye miili yao kusafirishwa kuelekea
kwenye mikoa yao kwa mazishi ambapo Katibu Tawala wa mkoa Kigoma,Injia John
Ngunguru aliongoza viongozi wa serikali na kamati ya ulinzi ya usalama kuaga na
kuisindikiza miili hiyo akimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma.
EmoticonEmoticon