MUME WA MTU ANASWA GESTI AKILAWITIANA NA SHOGA LIITWALO ' AUNT STEVE"


MWANAUME mmoja aliyefahamika kwa jina la Ezekiel Malika 'Baba Kulwa' amenaswa gesti na mkewe akiserebuka na shoga aitwaye Aunt Steve na kuibua mtiti mzito..

Tukio hilo lilivuta umati lilijiri Mei 20, mwaka huu kwenye gesti moja  iliyopo Mwananyamala, Dar ambapo mke wa Ezekiel alivamia na kutembeza mkong’oto wa hasira kwa mumewe.
 
Mei 19, mwaka huu, saa 3:15 asubuhi, mwanamke mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya heshima yake mtaani alilipigia simu gazeti hili na kutoa malalamiko kwamba mumewe amekuwa na tabia ya kulala na wanaume wenzake ambao ni mashoga.

“Jamani, mimi naitwa… (akataja jina), naomba jina langu lisiandikwe . Malalamiko yangu ni kwamba, mume wangu amekuwa na tabia ya kulala na mashoga, hivi ninavyoongea ana ahadi ya kukutana na mmoja wao gesti kama si kesho basi keshokutwa, niliona meseji kwenye simu ya mume wangu.

“Nawaomba chondechonde, mnisaidie ili hii tabia ikome. Nipo tayari kusikia maelekezo yenu ,” alisema kwa masikitiko mwanamke huyo.

Mratibu wa Oparesheni hii alimpa maelekezo mwanamke huyo akimtaka kufuatilia kwenye simu ya mumewe ili kubaini siku ya wawili hao kukutana gesti.

“Nawaahidi kwamba leo hiihii kabla giza halijaingia nitakuwa nimejua siku yao ya kukutana, naomba msiache kupokea simu yangu jamani.”

Saa 11:00 jioni, mwanamke huyo alipiga simu tena na kupokelewa na yuleyule mratibu wake aliyempa maelekezo.

Mwanamke: Mchana wakati mume wangu amekwenda kuoga niliipekua simu yake, wanakutana kesho kwenye gesti ya …(anaitaja jina).
“Kwa hiyo mtanisaidiaje?”

OFM: Wewe kuwa beneti na mumeo, kesho akiondoka na wewe ondoka hata kwa kujificha, mfuatilie hadi kwenye hiyo gesti huku ukitupa mawasiliano.

Mwanamke: Hilo halina shida, nitakodi Bajaj halafu nitawaambia.
 
OFM: Oke, kuwa makini, mawasiliano ni muhimu. Tutawanasa kisha wakaishie polisi. 

Mwanamke: Nitashukuru sana jamani. Loo! Kweli dunia imekwisha, mwanaume ana mke, hatosheki anatafuta wanaume wenzake, afadhali angekwenda kwa machangudoa.”

Siku ya tukio saa 8:00 mchana, mwanamke huyo akiwa ameongozana na mashoga zake, walifika kwenye gesti hiyo na kubana sehemu ambayo wangeweza kumwona anayeingia na kutoka kisha akawasiliana na mratibu wa OFM ambaye aliwatuma wapekuzi watatu wenye kamera za kupiga picha kwa umbali wa mita 100.
 
Kufumba na kufumbua, Aunt Steve aliwasili na kuzama ndani ya gesti hiyo kwa kutumia mlango wa nyuma ili asionekane kwa vile sheria ya serikali kuhusu gesti, wanaume hawaruhusiwi kuingia kwenye chumba kimoja.
wapekuzi  wetu wakiwa tayaritayari walitega katika pembe tatu za gesti hiyo ili kunasa tukio hilo hatua kwa hatua.

Kufumba na kufumbua, Baba Kulwa alitokea na kuingia ndani ya gesti hiyo kwa kutumia mlango mkubwa wa mbele huku akiwa hajui kama arobaini yake ilikuwa imebakiza dakika chache siku hiyo.
 
Alifika mapokezi na kupewa chumba No. 01, akaenda uani na kufanya jitihada kubwa za kumpitisha shoga huyo kwa mlango wa nyuma hadi ndani.

Baada ya wote kuzama chumbani, mke wa mwanaume huyo, mashosti zake na wapekuzi  waliwaacha kwa dakika kumi ili wafikie hatua ya kuchojoa nguo hivyo kuweza kuwanasa wakiwa watupu.

Baada ya dakika kumi, wafumaniaji wote walizama ndani na kugonga mlango wa chumba walichomo wawili hao huku shosti mmoja wa mwanamke huyo akijitambulisha yeye ni mhudumu anawaongeza taulo. Baba Kulwa bila kufahamu janja hiyo alifungua mlango kidogo na kuchomoza kichwa lakini ghafl a akinadada hao akiwemo mkewe walimvamia na kusukuma mlango, wakazama ndani.

Wawili hao walikutwa hawana nguo, ndipo msala ulipomwangukia Baba Kulwa na Aunt Steve wake, mke akipewa nguvu na wapambe wake waliwatembezea kipigo huku wakiwakejeli kwa tukio hilo la aibu.

Baada ya kuwaweka wote chini ya ulinzi, waliwatoa nje huku Baba Kulwa akiomba msamaha kwa mkewe lakini bila kukubaliwa.

“Msamaha wa nini? We si kidume cha kweli, twendeni nje tukawaanike mbele ya watu,” alisema mwanamke huyo.
 
Katika hali iliyoonekana ni kukosa umakini wa kuweka kizuizi vizuri, Aunt Steve alifanikiwa kuchoropoka kama samaki aina ya kambale na kutokomea kusikojulikana huku wanawake hao wakimsindikiza na zomeazomea hadi wakafunga mtaa.

Taarifa za katikati ya wiki iliyopita kutoka nyumbani kwa Baba Kulwa zilidai kuwa baada ya kufi ka nyumbani, mwanamke huyo alikusanya kila kilicho chake na kutimka zake huku mumewe akimbembeleza bila mafanikio

GPL
Previous
Next Post »