Viongozi
wa vyama vya siasa vitano AFP, UMD, CHAHUSTA, JAHAZI ASILIA NA
DEMOKRASIA MAKINI kwa pamoja tumeungana kutoa wito kwa wanasiasa
wenzetu, viongozi wa dini na wananchi wote kwa jumla kuhusiana na
uchaguzi huu unaotarajiwa kufanyika ifikapo tarehe 25/10/2015
Tamko hili ni pamoja na:-
1. Tunawapongeza wagombea wote wa nafasi ya Urais kwa kuendelea kufanya kampeni kwa njia ya amani na Utulivu.
2.
Tunawataka watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa
wingi siku ya tarehe 25/10/2015 kupiga kura kwa kuchagua viongozi
wanaowataka kwa amani na Utulivu.
3.
Viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali, Urais,
Ubunge na Madiwani waache kutoa maneno ya kuwatia hofu wapiga kura
kwamba tunaweza kuibiwa kura na badala yake tuwahamasishe zaidi
kujitokeza kwa wingii kupiga kura na kuiamini tume ya taifa ya uchaguzi
kuwa watatenda haki kwa wagombea wote bila kujali hadhi ya chama cha
siasa anachotoka mgombea.
4.Viongozi
wa dini wanaotaka kuwafanyia kampeni wagombea wasifanye hivyo katika
nyumba za ibaada na badala yake wakipenda kufany ahivo watumie majukwaa
ya kisia sa na sio madhabahu.
5.Viongozi wa vyama vya siasa waache kutoa vitisho kwa wapiga kura kwa kuwatia hofu ya kutabiri kuwepo kwa umwagikaji wa damu.
6.
Viongo wa asasi za kiraia wasiendelee kufanya tafiti na kuwapa ailimia
wagombea kiushabiki bila ya kufuata maadili na kanuni za kitafiti mabyo
matokeo ya tafiti zao zimekuwa zikileta mtafaruku katika jamii kwa kueta
za ama kumdhoofisha mmoja kati ya wagombea waliotajwa katika tafiti
husika.
7.
Mwisho tunawataka watanzania wote kuwa makini na kuyadharau matamko
yote yenye nia ya kuwatia hofu na kuendelea kuipenda nchi yetu ya Aamini
na Utulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa Taifa letu. Na
vilevile viongozi wa dini waendelee kuliombea taifa letu libaki kuwa na
utulivu wakati wote wa uwepo wetu katika nchi yetu.
EmoticonEmoticon