Mkurugenzi wa Mifumo Juhn Mlingi kutoka Taasisi ya
Mabasi yaendayo Haraka (Dar es Salaam Rapid Transport) akitoa ufafanuzi wa
maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kwa wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania
(Tanroads) na waandishi wa habari walipokuwa katika ziara ya kukagua miundo
mbinu ya mradi huo katika kituo cha Kivukoni jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads wakipanda gari la Mradi
wa Mabasi yaendayo Haraka jana jijini
Dar es Salaam katika ziara ya kukagua
Miundo Mbinu ya Mradi wa DART kabla ya kuanza kutumika .
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads wakikagua kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Kimara
ambacho ujenzi wake umekamilika
kwa asilimia mia moja jana jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Afisa wa
Tanroads akikagua kibanda cha kukatia tiketi kilichopo ndani ya kituo cha Kimara
katika mradi wa mabasi yaendayo haraka wakati wa ziara ya ukaguzi wa miundo
mbinu ya mradi huo jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanyakazi wa Tanroads wakiwa ndani ya moja ya
mabasi ya mradi wa mabasi yaendayo haraka walipokuwa wakifanya ziara ya kukagua miundo mbinu ya mradi huo
jana jijini Dar es Salaam.
Na Ally Daud- MAELEZO.
Wafanyakazi wa Mradi wa Mabasi ya endayo haraka Dar es salaam
(DART ),Wakalawa Barabara(TANROADS) pamoja na Umoja wa wamiliki wa Daladala Dar
es Salaam (UDART) wamefanya ziara ya kufahamu na kuelewa miundo mbinu ya mradi huo.
Akizungumza na waandishiwa Habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi
wa Mifumo DART Bw. Junn Mlingi alisema mabasi hayo yatatumia dakika 45 mpaka 35
kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kutumia dakika mbili kusimama
kila kituo ili kuruhusu basi lingine lifike katika kituo husika baada ya dakika
tano.
“Mradi huu unatarajiwa kukabidhiwa mnamo Novemba mwaka huu kwani
mpaka sasa mradi umekamilika kwa asilimia 80 katika kipindi cha kwanza ambapo unaanzia Kivukoni mpaka Kimara mwisho na
Sheria ya matumizi ya miundombinu ya DART
ipo na inasema kwa yeyote atakayekamatwa akihujumu miundombinu atatozwa faini
ya shilingi laki tatu au kutumikia kifungo cha miezi sita hadi mwaka mmoja ama kutumikia
adhabu zote mbili”, alisema Bw. Mlingi.
Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Bw. Mlingi alisema waratibu
wa mradi huo wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora za usafiri kwa wananchi
na wakazi wa jiji la Dar es salaam kwa kuboresha sheria , taratibu na miundombinu
itayotumika kutumia usafiri huo wa mabasi yaendayo harakakatika barabara zake maalumu.
Aidha Mratibu wa Mji DART Bw. Edwin Hema alisema Mabasi hayo yatakua
yanatembea kwa mwendo wa kawaida kwa kilomita 50 kwa saa ikiwa ni kasi ya juu na
kilomita 20 kwa saa ikiwa ni kasi ya wastani kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo
cha Kimara na kuwa na muda maalumu wa kushusha abiria na kupakia.
Mbali na hayo Bw.Hema alisema wananchi hawatatakiwa kugombania
mabasi kwani yatazingatia muda uliyopangwa katika taratibu zakubeba abiria na
pale gari itakapohitaji kusimama dereva atatangaza kituo na abiria watatakiwa kukaa
mbali na mlango mpaka milango itakapofunguka.
Naye Mkurugenzi wa Mifumo alisema wameweka utaratibu kwa walemavu
wote watakaotumia usafiri huo kwa urahisi na haraka na kuweza kuwahi kwenye shughuli
zao bila yausumbufu kwa kuwa wana sehemu zao za kukaa na kwa wale wanaotumia baiskeli
za kusukumwa wataweza kupanda na baiskeli zao ndani ya basi hilo.
Kwa upande wa Msemaji Mkuu wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala
Dar es Salaam (UDART) na mradi wa mabasi hayo Bw. Sabri Mabruki amesema mpaka sasa
wameingia mkataba wa kuleta mabasi 76 ya kuanzia kupitia Kampuni ya Golden Dragon kutoka Japan.
EmoticonEmoticon