Kijana aliyekamatwa na polisi kwa ajili ya kuleta saa aliyoitengeneza
iliyodhaniwa kuwa bomu aachiliwa na kupata mwaliko rasmi kutoka kwa rais Obama
katika Ikulu ya Marekani
Ahmed Mohamed ni kijana wa umri wa miaka 14 anayeishi Texas alishutumiwa na maafisa wa
polisi kutengeneza bomu.
Wakati huo huo, mkurugenzi wa Facebook
Mark Zuckerberg pia alimwalika Ahmed kumtembelea katika kampuni yake iliyokuwa
makao makuu yake Carlifonia.
Mark pia aliandika ujumbe kwenye Facebook ulisoma,
‘‘Umiliki wa kipaji cha ubunifu wa kuunda kifaa kizuri unapaswa kuleta sifa na
wala sio kukamatwa.’’
Tukio la kukamatwa kwa Ahmed limezua gumzo kwenye mitandao ya
jamii na kupelekea kuanzishwa kwa kampeni ya #IStandWithAhmed katika jukwaa la Twitter.
Baraza la mambo yanayohusiana na dini ya kiislamu Marekani lilishutumu
vikali tukio hilo na kusema kuwa ni mfano tosha wa chuki kwa waislamu nchini.
Hata hivyo msemaji wa polisi James
McLellan alikanusha madai ya baraza hilo na kusisitiza kwamba dini ya Ahmed haikuwa na uhusiano wowote
na kitendo chao cha kumkamata kijana huyo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani
Josh Earnest alisema kuwa Ahmed amealikwa katika Ikulu hiyo ili aweze kushiriki
katika elimu ya nyota pamoja na wanaanga wa NASA.
EmoticonEmoticon