Meneja
mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati alipokuwa
akijitambulisha, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim
Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Meneja
mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, alipozungumza nao, kuhusu
mafanikio na matarajio ya shirika, wakati akijitambulisha, Dar es Salaam
jana.
**************
Na Mwandishi wetu
SHIRIKA
la Ndege la Kimataifa Emirates lenye makao yake makuu Dubai, jana
lilimtangaza Meneja wake mpya wa Tanzania Bw. Husain Alsafi.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa hafLa fupi ya utambulisho wake
Mtendaji huyo mpya wa Emirates Bw. Husain Alsafi alisema kwamba,
Emirates imefanikiwa kufikia wastani wa asilimia 12% wa idadi ya wateja
wake wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu.
Mtendaji
huyo mkuu aliongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa Shirika hilo la Ndege
la kimataifa linatimiza matakwa ya abiria wake hasa kwa soko la Tanzania
na kwingineko, hivyo basi wameahakikisha kuwa na safari za kila siku
kutoka Tanzania kwenda nchi za nje kupitia Dubai, hivyo watanzania wengi
wananufaika pale wanapotumia kusafiri na shirika hilo ambapo pia
wanapata faida Zaidi endapo watapanga safari zao mapema ili kupata
punguzo la bei/nafuu Zaidi.
Katika
kushiriki kwake Tanzania Mtendaji huyo MKuu alisema kuwa wametoa
kipaumbele kikubwa kwa wazawa ambapo katika kuajiri wamefanikiwa kuwa na
watanzania Zaidi ya 30 katika shirika hilo na pia wanazidi kuongeza
idadi ya Watanzania ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi Zaidi.
“
Emirates Tanzania imefanikiwa kuajiri watumishi wengi sana kutoka hapa
hapa nyumbani ikiwa ni mojawapo ya vipaumbele vyetu katika kila nchi
husika na pia tunaendelea kutoa nafasi mbali mbali Zaidi”, alisema Bw.
Alsafi.
Kuhusu
kupanua vituo Mtendaji huyo alisema kuwa Emirates imeendelea kuwa
kivutio cha utalii duniani kwote kwa njia mali mbali ikiwa ni pamoja na
kuongeza/kupanua vituo vyake sehemu mbali mbali ambapo kwa mwaka huu
hali hiyo imepelekea kukua kwa soko lao hasa kwa nchi kama vile India,
UK, Amsterdam, China na France, sehemu ambazo watalii wengi wamekua
wakivutiwa Zaidi pindi wanapofanya safari zao kupitia shirika hilo la
Ndege.
Akizungumzia
kwa upande wa kusafirisha mizigo mbali mbali aliongeza kuwa Emirates
imekua ikifanya kazi kwa ukaribu sana hasa na wakulima wa Tanzania kwa
muda mrefu sana, ambapo kupitia kitengo cha Sky Cargo kimekua mstari wa
mbele katika kutimiza hilo na kuhakikisha usalama wa mizigo ya watu pia
kuwafikishia kwa muda uliopangwa, kuwaunganisha wafanya biashara kutoka
Tanzania na wale walioko nchi zingine kama Arabuni (UAE) n.k. kudhamini
Watanzania wanaozalisha na kusafrisha bidhaa zao za chakula katika
maonyesho Dubai.
Wanawapatia nafasi ya kukutana na kuzungumzia maendeleo a wanunuzi mbalimbali ulimwenguni.
EmoticonEmoticon