Taarifa Rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imetolewa na inahusu hali ya Watanzania ambao wako Mecca kwa ajili ya Hijjah… Taarifa hiyo inasema hakuna Mtanzania yoyote ambaye amejeruhiwa wala kuumia kutokana na ajali hiyo.
Idadi ya watu waliofariki ni 107 na wengine 200 wamepata majeraha… MUNGU awapumzishe kwa amani wote waliofariki na awape nafuu pia wote waliopata majeraha kwenye ajali hiyo.
Hapa ninazo picha kutoka MICHUZI BLOG ambazo zinaonesha baadhi ya Watanzania walioko Mji wa Mecca, Saudi Arabia… kati yao yumo pia Mchekeshaji na Mwigizaji King Majuto.
EmoticonEmoticon