Kampuni ya StarTimes Media ya jijini Dar es salaam leo imeingia
mkataba wa udhamini na TFF kudhamini Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL)
inayoshirikisha timu 24 kutoka katika mikoa 16 ya Tanzania bara.
Akiongea na waandishi wa habari wakai uwekaji sahihi mkataba huo,
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi
ameshukuru kituo cha Star Times kwa kuamua kuwekeza katika mpira wa
miguu na hasa kwenye chimbuko la vipaji na wachezaji wengie nchini.
Malinzi amesema udhamini huo wa shilingi milioni 900 kwa kipindi cha
miaka mitatu, unatarajiwa kuongezeka wiki ijayo baada ya kuingia mkataba
na mdhamini mwingine wa kurusha matangazo ya ligi hiyo kwa shilingi
milioni 450 na kufikia jumla ya udhamini wa shilingi bilioni 1.3.
Aidha Malinzi amesema TFF inaendelea na mipango ya kuhakikisha
inavisaidia vilabu vya madaraja ya chini, timu za wanawake na vijana
kuona vinapata udhamini na kuweza kushirki vyema michuano mbalimbali.
Naye Mkurugenzi wa StarTimes Media nchini, Lanfang Liao amepongeza
ushirikiano mpya ulioanzishwa kati ya kampuni yake na TFF na kuahidi
kudumisha ushirkiano huo kwa faida ya maendeleo ya mpira wa Tanzania.
Mwenyekiti wa timu ya Kinondoni Municipal Council (MKC), John Njunde
akiongea kwa niaba ya vilabu vya ligi daraja la kwanza, amesema
anaishukru TFF kwa kuweza kuvitafutia udhamini vilabu na sasa wataweza
kushiriki vizuri ligi hiyo inayotoa timu tatu zitakazopanda ligi kuu
msimu ujao.
EmoticonEmoticon