Polisi
nchini Argentina wamemfungulia mashtaka mwanaume mmoja ambaye anadaiwa
kumfungia kwenye chumba mkewe pamoja na mtoto wake mkubwa wa kiume kwa
miaka kadhaa kama wafungwa.
Polisi
wamesema chumba hicho kichafu chenye harufu mbaya kilichopo kwenye
nyumba ya Bw. Edgardo Oviedo katika mji wa pwani wa Mar del Plata kina
mlango wa chuma na kufuli kwa nje.
Pia , walikuta vyakula vya mbwa, ambavyo inaaminika kuwa alikuwa akimpatia mkewe huyo na mtoto wake wa kiume.
Polisi wamesema mkewe amekutwa na matatizo ya akili na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 33 hawezi hata kuzungumza.
-BBC
EmoticonEmoticon