MWAMNYANGE AZINDUA BARAZA LA USHAURI TCAA


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamyange akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ushauri wa Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC) na semina ya wadau wa usafiri wa anga Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamyange akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Baraza  la Ushauri wa Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC, Shaban Mtambalike wakati wa uzinduzi wa baraza hilo la nne tangu kuanzishwa kwake. 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri wa Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC), Hamza Johari akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi huo. 

 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu-Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamnyange (walioketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza hilo na wadau wa Sekta ya usafiri wa Anga.
****************
Na Father Kidevu Blog
USHINDANI mdogo katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga kutokana na kuwepo kwa mashirika machache ya ndege yanayotoa huduma nchini.

Hayo yalibainishwa Dar es Salaam jana na  Katibu Mtendaji wa baraza la Ushauri wa Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC), Hamza Johari wakati wa uzinduzi wa baraza hilo na semina kwa wadau wa usafiri wa anga nchini.

Johari alisema endapo kama nchini kungekuwa na watoa huduma wengi wa usafiri wa anga basi kungepelekea kushuka kwa gharama za usafiri na kuwepo kwa huduma bora miongoni mwao.

“Siku zote tunaamiani kama ushindani wa kutosha gharama zinakwenda chini, huduma zinakuwa bora, na ni mdogo kwasababu soko na miundominu haijaweza kutandaa nchi nzima, ”alisema Johari.

Aidha Johari alisema pindi nchi itakapokuwa na miundombinu bora ya viwanja vya ndege, na utaratibu mzuri wa huduma za anga nchini anaamini huduma zitaboreka zaidi.

Mapema akifungua baraza hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamunyange amewataka kuwa karibu na wadau wa sekta ya usafiri wa anga nchini ili kuweza kutoa huduma bora na zenye ufanisi nchini.

Mwamunyange alisemwa ipo haja ya baraza kulifanyia kazi dhana ya ushirikishwaji na utoaji wa elimu kwa walaji kuwa ya vitendo zaidi.

“ Baraza linatakiwa kuwashirikisha wadau wake katika mambo mbalimbali yanayoendelea katika seklta nzima ya usafiri wa anga lakini pia wanapaswa kutoa elimu ya mara kwa mara ya haki na wajibu wa mlaji,”alisema Mwamunyange.

Baraza lina takiwa kuangalia maslahi ya mtumiaji wa huduma za usafiri wa anga na kutoa elimu ambayo itamfanya mlaji awe na uwelewa wa kutosha wa huduma za anga.

Aidha Mwamunyange amesema kwa sasa huduma za usafiri wa anga nchini zinakabiliwa na changamoto kutoka kwa walaji ambapo wanashindwa kutofautisha huduma zitolewazo na mashirika yatuayo huduma za gharama nafuu nay ale yaliyozoeleka.

Wadau wa usafiri wa anga pia walipata fursa ya kushiriki semina baada ya uzinduzi huo na mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na huduma kwa wateja, uwajibikaji wa mtoa huduma anaposababisha madhara, ndege za bei nafuu na masuala ya usalama.

Uzinduzi wa baraza hilo la nne la Ushauri wa Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC), baada ya kuteuliwa na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta ambapo pia wajumbe wa Baraza lililopita waliagwa.
Previous
Next Post »