ASKARI ALIYEUWAWA NA MAJAMBAZI AAGWA LEO JIJINI MBEYA


Mwili wa marehemu askari polisi a namba  G 2526 DC Willium Juma aliyeuwawa na majambazi June 10 mwaka huu ukiwasili nyumbani kwake ghana kwa ajili kuagwa.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kifo cha askari huyo.


Ndugu na jamaa wakiomboleza msiba huo nyumbani kwake ghana leo June 11

Mwili wa marehemu ukitolewa ndani tayari kwa kuagwa na ndugu na jamaa


Mke wa marehemu akifarijiwa









Marehemu DC Willium Juma enzi za uhai wake

Mkuu wa wilaya  ya mbeya Nyiremba Munasa akitoa salamu katika msiba huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akizungumza katika msiba huo



.
ASKARI polisi namba  G 2526 DC Willium Juma, ameuawa kwa kupigwa risasi ya kifua na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.

Marehemu, Juma inasemekana alikutwa na mauti hayo akiwa njiani akikimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.

Akizungumza  wakati akiaga mwili  marehemu  , Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema marehemu Juma alipatwa na mauti hayo akiwa njiani akikimbizwa hospitali baada ya kupigwa risasi ya kifua na watu wanaosadikiwa ni majambazi.

Amesema, marehemu Juma pamoja na wenzake, wakiwa katika doria ya mchana walipata taarifa  ya wahalifu hao  ambao inasemekana walikuwa katika harakati za kuwavamia raia wa kihindi wamiliki wa Kampuni ya Export iliyopo katika eneo la Iwambi jijini Mbeya.

Alisema, inasemekana wahindi hao walikuwa wametokea Benki  kuhifadhi fedha zao hivyo majambazi  walihisi kwamba wahindi hao walikuwa wametoka kuchukua fedha  hivyo kutaka kuwapora kwa kutumia silaha.



Kamanda Msangi, amefafanua  kuwa, wakati askari wakiwa wanaangali mbinu za kuingia kwenye eneo ilipotokea milio ya risasi, walishangaa kuona pikipiki mbili zikiwa zimepakia watu zikija kwenye eneo lao .

Alisema, inasemekana pikipiki moja iliwapita askari hao nay a pili ilisogea na ndipo jambazi mmoja alitoa silaha yake na kumimina risasi hovyo ndipo moja ilimpata marehemu Willium katika kifua chake na kumsababishia mauti yake.

Amesema,  jambazi huyo alipopigwa risasi ya mguu alifanikiwa kukimbia lakini alishindwa kuendelea na safari yake kutokana na kupoteza damu nyingi hivyo askari kufanikiwa kumkamata na alipoulizwa jina lake alijitambulisha kuwa anaitwa peter na kukata roho hapo hapo.

Aidha, Kamanda Msangi, amesema jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha moja iliyotengenezwa kwa kienyeji  ikiwa na risasi mbili zinazotumika kwenye bunduki aina  ya Shot gun na kwamba msako unaendelea kwa ajili ya kuwakamata waliofanikiwa kukimbia pamoja na silaha moja.

Hata hivyo alisema kuwa mwili wa Marehemu Willium juma, unasafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Mkoani Mara kwa ajili ya maziko, huku mwili wa  jambazi ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya.

Mwisho.
Previous
Next Post »