SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?

Displaying sehemu ya 32.jpg

MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no,0755683295/Watsap, instagram@mwalim_yuu, fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email@yusuphngahala@gmail.com.

SEHEMU YA 32.
Tulipoishia, Nikamfikia na kumbana vizuri kisha nikamnyonga bila kuchelewa. Kisha nikamlaza mle ndani nikaanza kutoka kurudi nje. Lakini wakati nageuka ili nipotee eneo lile nikasikia sauti ikisema kijana_______Enda nayo.......... Hebu tulia hapo hapo. Niliinua kichwa na kumwona ni mfungwa mmoja mwenye kifua kimejaa na mikono ilijaa. Alikua na midevu ya kutisha mweusi kama mkaa. Sura ya ugaidi ilikua inajidhihirisha alikua anavuta bangi bila wasiwasi. Nikamsikia akiendelea. Sauti ilikua nzito sana mpaka niliogopa. Akasikika nimekufuatilia mda mrefu sana tangu umefika hujamaliza hata wiki ila una mambo makubwa sana.

Je utakuwa tayari nikusaidie kitu kimoja. Nikamjibu enheee sema. Akasema sikia humu ndani wengine sisi siyo wafungwa mimi nina kazi humu ndani ninatafutaga vijana wenye nguvu kisha nawasaidia kutoka humu na wakitoka kuna kazi watanisaidia huko nje chini ya boss wangu. Je uko tayari nikutoe humu mana naona uko vizuri uko tayari? Nikajua tuu hawa ni sehemu ya majambazi wa hapa Tanzania hivyo kukubali ilikua ni njia rahisi ya kuonana na Zabroni Makweka. Nikamwambia nipe mda akajibu sawa.

Kisha akanipa kibulungutu cha fedha zilikua noti za elfu kumikumi. Niliziangalia kisha nikatoka bila kuchukua. Aliniangalia kwa jicho lisiloamini kilichotokea. Nilirudi ndani mda ukazidi kusonga siku zikapita huku nikizidi kuwamaliza wabaya wangu mle jela kimyakimya. Sitasahau siku niliitwa na maaskari magereza wakaniuliza juu ya mauaji ya mle gerezani nikakubali kwa ujasiri na kujiamini kua mimi ndiye ninayeua kila siku. Wakaniuliza sababu nikajibu Kwa fujo huku nikiwa na jaziba. Haki haki iko wapi haki? Eti nchi ina sheria sheria zipi zisizoona zipi?

Tazama nilifungwa bila hatia sikusikilizwa. Mke wangu alibakwa na wanaume sita, mwanangu mdogo alilawitiwa na wanaume sita haohao kisha kumuua kikatili. Mpaka sasa hakuna aliyeenda jela hata mmoja hata kukamatwa. Nimeingizwa jela kupisha uchafu wa watu wachache uendelee. Nakuja jela nimelawitiwa nimeumizwa vibaya sehemu za haja kubwa. Lakini hakuna hata askari mmoja kati yenu aliyechukua hatua. Je hamkujua mimi ni binadamu na nimepoteza utu wangu. Thamani yangu iko wapi? Halafu mnakaa hapa mnapiga kelele eti HAKI humu ndani kuna vitu vingi visivyopaswa kuwemo sigara, bangi, madawa ya kulevya, silaha kama visu, sindano za sumu watu wanamiliki askari mko wapi mko wapi askari halafu mnakaa kusema kuna sheria zipi?

Mmekaa hapa kunihoji kwanini naua mnataka kujua kwanini naua? Niliinuka na kumkuda askari mmoja nikamwinua juujuu nikamtupa huko. Hali ile iliwafanya wengine waogope. Wakatoa bunduki zao na kunielekezea. Nikiwa nimefura kwa hasira na uchungu macho mekundu yakitiririsha machozi ya hasira. Mikono ilikua ikitetemeka kwa hasira. Nikapayuka kwa nguvu mnadhani naogopa kufa? Niueni piga hata risasi mia piga piga piga!!!! Nilikua nikipayuka huku nikimfuata askari mmoja. Kisha nikashika bunduki yake nikaielekeza kichwani kwangu nikamwabia fyatua risasi. Siogopi risasi wala simwogopi mtu.

Nchi imewaamini imewaweka mlinde wafungwa mnalipwa mishahara. Mnasimesha watoto mnatanua na familia lengo mlinde wafungwa kwanini mnafanya uchafu. Kwanini mnakosa haya? Kwanini mnatumia vibaya pesa za walipa kodi? Kwanini? Halafu mnakaa hapa na kuongea kama kasuku HAKI mnajua nini maana ya Haki? Haya niuweni sasa. Maneno yale yaliwafanya wakose nguvu na ujasiri kisha wakaingiwa na woga kiasi. Nikapita katikati yao kurudi gerezani. Wakati naingia nilikutana na yule njemba aliyekuwa akinifuatilia. Nilikua nina hasira mbaya. Kitendo cha kunisemesha kiliniudhi nikajikuta namrukia na kumpiga kiwiko cha kichwa. Alianguka kama zigo puu! Kisha mi nikasonga mbele. Wafungwa wengine wakawa wanapisha njia na kuniacha nipite.

Kimya kilitawala kila mmoja akiniangalia bila kuamini. Sikutaka kusemezana na yeyote nikafika sehemu yangu ya kulala nikalala. Gereza zima lilitulia tulii. Baada ya mda kupita hasira zilipungua nikainuka na kutoka nje walau nikaotee jua. Sikua na rafiki wala niliyejuana naye jela nzima. Walikuwepo niliowahi kuwakamata miaka ya nyuma wakajaribu kuleta ubabe niliwafunza adabu bila huruma. Hali ile ilinifanya kila mtu kuniogopa. Nilikua na nawazo mengi sana. Niliwaza mama na baba yangu hali zao za maisha nikakumbuka mambo mengi sana nikaishia kulia.

Hakuna anayezaliwa muuaji wala mkosaji lakini hali inaweza ikakufanya ukawa gaidi. Sikuwahi kuwaza kama kuna siku mimi nitanyonga watu kwa kutetea haki yangu. Sikuwahi kuwaza kama nitaogopwa kwasababu ya ubabe na uuaji ulionitawala mda mfupi ndani ya jela. Haki ilinifanya nibadilike. Sheria ilipindishwa na kunihukumu bila kosa. Madhara yakaonekana gerezani. Nilikata tamaa ya maisha sikuwa naogopa lolote hata wangelisema nitanyongwa kwangu ilikuwa sawa tuu. Maisha yalikua yamebadilika sana. Nilijua huenda nitaongezewa mda wa kifungo kwasababu ya kuua ovyo lakini haikua hivyo. Taratibu hata askari magereza walianza kuogopa kuvunja sheria. Wafungwa pia wakawa wanajiheshimu.

Nilileta mabadiliko ya mda mfupi ndani ya jela. Siku zikasogea na kwenda kasi hata yule aliyepanga kunitorosha sikumwona tena. Niliapa kumaliza kifungo changu kisha kutoka kwa amani na nitokapo huko nje wabaya wangu wajipange. Ilikua ni huzuni sana kwangu lakini nifanya nini unadhani. Tangu kufungwa hakuna hata askari mmoja aliyewahi kuja kuniangalia. Sikulijali sana hilo. Kuna siku baada ya kipindi kirefu nilishangaa naitwa eti kuna wanahabari wamekuja kunihoji jela. Nilitoka ndipo nikakuta maiki na kamera mbalimbali zikiwemo za BBC,TBC,ITV,STAR TV, CHANEL FIVE, CHANEL TEN, CLOUDS FM, na nyingine nyungi.

Baada ya kukaa wakaanza kunipiga picha na baadhi kunihoji maswali yao yalikuwa ya ajabu kidogo. Bwana Yusuph Ng'ahala ulifungwa kwa tuhuma za ujambazi na mauaji lakini tangu kufungwa kwako bado unaonekana kuua na kufanya ujambazi nje je hua unatoroka jela? Lilikua swali la mwandishi wa gazeti moja. Nikajibu kwa gadhabu sijui. Mwingine akadakia je unahisi hukumu ilikustahili hiyo nikajibu hapana nilipaswa kufungwa kifungo cha maisha. Sasa mbona umefungwa na pia mtu huyohuyo unaonejana ukiua na kuiba au kuna namna? Nikajibu kwa hasira hua naiba jela? Mmenikuta jela na sijawahi kutoka tangu nifungwe na mnaniuliza juu ya kuua nje ya jela mi ni mzimu? Najigawa? Au mimi ni jini? Mmoja akajibu sasa anaeonekana nje ni nani nikajibu kwa mkato Zabroni Makweka.

Eeee huyo Zabroni ni nani? Nikajibu kwa hasira si ndiye Zabroni makweka. Kwakuwa sikuona umuhimu wa yale mahojiano nikainuka na kuondoka. Nilipigwa picha nyingi sana na waandishi kisha nikarudi ndani. Sikutaka kufuatilia wala kuonyesha ushirikiano na vyombo vya habari kwani walikuwa wapi siku zote nahukumiwa? Tuliwahi kabla kuwaita na kuwataarifu juu ya uwepo wa mtu anayefanya mauaji na uporaji alikua na mwonekano kama wangu je mbona hawakulifikisha popote? Sikuona faida ya lolote kwakweli nilamua kutulia ninalize kifungo na nitokapo nikamalize kazi kisha nifungwe mara ya pili.

Siku zilisinga na kusogea huku mle jela haki ikiimarishwa. Amini kijana ukijiamini unaweza kua chachu ya mabadiliko mahali popote. Ukimya na upole wangu uliwafanya wafungwa wanidharau wakati nafika. Lakini kupigania haki yangu na kutokumwogopa mtu na kujitoa muhanga kuliwafanya wengine kupata haki zao na askari kubadilika lakini chanzo ni mimi! Nilikuwa naogopwa na mimi sikutaka rafiki yetote mle ndani. Ilikua inafika hadi mwezi sijafungua kinywa changu na kuongea na mtu. Kuna siku tukiwa ndani mimi nilikaa peke yangu kama kawaida wenzangu walikuwa vikundi vikundi. Walikuwa wanaingizwa wafungwa wapya. Sikuamini macho yangu ninachokiona ukisikia Mbuzi kafia kwenye kibanda cha supu ndio hii. Niliinuka kwa mshangao Pale nilipomwona___________________

______________________________________________________________________________________________________________________________________Je yuu alimwona nani? Cheki na mm sehemu ya 33 kwa llte mawasiliano hayo hapo juu nawapenda wote
Previous
Next Post »