TATIZO la usafiri katika
Jiji la Dar es Salaam linatarajia kupungua baada ya mabasi 138 ya Mradi
wa mabasi Yaendayo Haraka (BRT) unaotarajiwa kuanza kazi Oktoba 2 mwaka
huu kuwasili katika Bandari ya Dar es Salaam yakitokea China. Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki amekuwa mmoja wa mashuhuda,
baada ya kujionea mabasi hayo alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam
jana. Akizungumza baada ya kuyaona
bandarini Dar es Salaam, alisema: “Tumefikia hatua nzuri na naipongeza
Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDART) kwa kuleta mabasi hayo kwa ajili ya
kuanza kutoa huduma hii ya usafiri katika kipindi cha mpito. Hii
itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji hili.” Alisema
kampuni hiyo imepewa jukumu la kuendesha kipindi cha mpito ili waweze
kupata uzoefu na zabuni ya mwendesha mradi kipindi cha kudumu itakapo
tangazwa itasaidia wao kushindana. Aliongeza kuwa, Serikali ilifanya
kazi kubwa kuunganisha Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wamiliki wa
daladala na baadaye kuanzisha kampuni ya UDART. Aidha alikanusha kuwa
nauli za mabasi hayo imepangwa kuwa Sh 900 zilizotolewa katika mtandao,
na kusema huo ni uzushi na upotoshaji na aliyefanya hivyo anatafutwa ili
sheria ichukue mkondo. Alisema suala la nauli linahusisha ushiriki wa
taasisi mbalimbali chini ya Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi
Kavu (SUMATRA) hivyo uzushi huo umewaletea usumbufu mkubwa wakazi wa Dar
es Salaam hivyo wanatakiwa kuwapuuzia. Msemaji wa Kampuni ya UDA Rapid
Transit (UDA-RT), Sabri Mabrouk alisema mabasi yote yameingia yakiwemo
ya meta 12 yapo 101 na meta 18 yapo 39 na huduma ya usafiri kipindi cha
mipito itanza baada ya kukamilisha taratibu za bandari. “Tuliahidi kuwa
mwezi huu wa tisa mabasi yatakuwa yamewasili na ni kweli yamekuja,” na
kwa pamoja na yale ya kufundishia yatakuwa mabasi 140,” alisema Mabrouk
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon