SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?

Displaying Sehemu ya 31.jpg

MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no, 0755683295/Watsap, instagram@mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, emali@yusuphngahala@gmail.com.

SEHEMU YA 31.
Tulipoishia, Usiku ule ulizidi kusonga mara kukiwa kumetulia sana nadhani ilikua ni usiku mnene. Tayari baadhi ya wanaume walianza kutembea tembea mle ndani. Mara mimi nikashtuka nashikwa mikono na miguu kisha_______songa sasa..........Wakaniinua taratibu na kuanza kusogea na mimi pembeni. Kwakua nilikua macho nikaamua kulianzisha timbwili palepale. Nilijikusanya nikawavuta na kuwajaza katikati lakini wapi hawakuniachia. Nilifanya kila mbinu ikawa ngumu wao kuniachia. Hatimaye wakafika mahali penye uwazi na wafungwa wengine hawakuwako. Nilianza kuvuliwa nguo na huku wengine wakiwa bado wamenishikilia.

Nilifanya kila ujuzi ilishindikana. Walikua ni wengi kiukweli. Bahati mbaya katika purukushani mdomo wangu ulizibwa. Pili wafungwa hua na tabia moja mbaya wakisikia kelele huinua mashuka yao na kujifunika vizuri. Hili linasababisha uchafu ndani ya jela kuzidi kukomaa hatuna ushirikiano. Basi wakamaliza kunivua. Wengine wakanikandamiza chini kifudifudi nisiweze hata kufurukuta. Kwa mbali nilihisi kuingiliwa yani kulawitiwa. Ningefanya nini unadhani. Nilijikunja uwezo wangu wote niling'ata baadhi ya wale walionishika lakini haikusaidia kitu.

Hatimae niliumizwa sehemu ya hajakubwa vibaya. Walipokezana kunishika huku wakipokezana kunifanyia unyama huo. Niliumia sana nilivuja damu nyingi lakini nani angejali. Niliishia kuwakwarua na kucha na kuwang'ata waliokua wakiniziba midomo. Lakini haikua na msaada kwa pale. Walimaliza na kutimiza azma yao. Kisha kuna sindano nikadungwa na sikujua nini kiliendelea. Nilishituka asubuhi na wakati maaskari wakituamsha kwenda kupasuabkokoto. Nadhani nilichomwa sindano ya usingizi. Iliingiaje jela wakati ni mwiko. Hakika kuna tatizo sehemu katika usimamizi.

Wakati nataka kuinuka ndipo nilohisi maumivu makali sana. Nikajaribu kujikaza nikaona kabisa siwezi kusimama. Nikabaki nimelala pale. Afande alikuja na kunipiga kiboko sehemu ya makalio. Huyu alikua kama kagongelea msumari kwenye kidonda kibichi. Nilihisi mapigo ya moyo yamesimama na damu haizunguki sawa mwili wote. Mishipa ya fahamu ikapoteza kumbukumb. Nilikua katika hali mbaya. Niliumanisha meno kama ishara ya kuumia machozi bila kuyatafuta yalitoka.

Afande alihisi kitu akaniuliza we vipi? Nikaishusha suruali akaona jinsi nimeharibika. Akaamuru nikimbizwe hospitali. Nilifika hospitalini nikahudumiwa huku pingu iko mikononi. Nilihudumiwa kwa siku mbili kisha nikaruhusiwa niliweza kutembea japo kwa taabu kiasi. Nilifika jela huku maumivu yakiwa bado yananitesa. Pia nililia sana kwani mwanangu pia alilawitiwa kama mimi na kuuawa. Hivyo nilijikuta naingiwa na hasira za ajabu. Nilikumbuka kitu kimoja kua walionikamata wengi niliwang'ata na kuwakwarua na kucha. Niliamua jambo moja tuu kufuatilia yeyote mwenye yale makovu halali yangu. Nilipumzika kiasi.

Ulifika mda wa kuchukua chakula pale ndipo niliamua kufuatilia mikono ya watu. Nilikagua kimyakimya kama nisiyeona kitu hivi. Mara nikamwona mmoja ana alama za meno. Nikaikalili sura. Baada ya chakula cha usiku nilimfuata na kumshika nikamwambia ukipiga kelele halali yangu nifuate. Nikamshika mkono kisha nikaanza kupotea naye pale. Niliingia naye chokni nikamuhoji kwa adhabu kali akataja kundi lote lilohusika. Nikaanza na yeye. Nilimnyonga kwa kuvuta ba kupishanisha sgingo.

Alipoanguka chini mi.i nikatoka mle chooni na kisha nikamtafuta wa pili kwa kuwa nilielekezwa alipo nikamfuata na hapakuwa na watu nikamvizia na kuvuta shingo naye akapotea. Nilitoka usiku ule haukuwa wa amani kwangu nilikuwa nawaza mambo mengi sana. Thamani yangu kama binadamu iko wapi? Tazama nimelawitiwa na hakuna aliyeshuhudiwa akichukuliwa hatua za kinidhamu. Je nilikua nakosea kuwaua? Ningefanya nini unadhani zaidi ya hilo Kuua ndiyo njia pekee ilibaki kwangu. Mwanangu kalawitiwa. Mke wangu aliuawa akabakwa kwa njia zote zaidi na mimi!! Hii ilikua sasa imezidi niliona suluhisho ni kuua tuu.

Usiku ule niliamka na kupanga yeyete atakaefanya lolote la kipuuzi naua. Nilipita na kwenda chooni kulojoa kwanza nikakuta zile maiti za jioni hazipo. Nikatoka wakati natoka nilikutana na mtu ambaye alionekana wazi alinifuata mimi. Mara akanishika na kunivuta kurudi chooni kisha akasema kwa kunong'ona kaka unaonekana kama kuna watu unawatafuta siyo. Nilimwangalia juu mpaka chini nikamwangalia usoni kisha nikaondoka bila kumjibu chochote. Nikarudi kulala. Nilikua silali usingizi nilikua nawaza vingi sana. Usiku ule ulipita vizuri asubuhi kulipokucha kama kawaida tulipaswa kwenda kupasua kokoto.

Tulifika huko chini ya ulinzi mzuri. Tulifanya kazi vizuri sana. Mara kuna mtu nikamwona ana alama za meno mkononi. Halikuwa swala la kuuliza zaidi ya kumkalili sura ili afundishwe adabu. Nilimkalili sura kisha nikaendelea na shughuli za lale. Baada ya kurudi jela nilianza kumfuatilia ili afikapo eneo lenye utulivu kidogo nimmalize. Sikuwa hata nauliza. Nilikua na uchungu sana kwani nilikuwa nimedharirishwa sana sikuona tena thamani ya kuishi. Nilitamani kujiua lakini nikaapa mpaka nimuue mmoja baada ya mwingine. Kisha nitajiua na mimi pia.

Nilimfuata mpaka akafika sehemu flani nadhani alikua anataka kuvuta sigara. Kwasababu mle gerezani haziruhusiwi alilazimika kujificha hapo ndipo na mimi nikatumia vizuri nafasi ile. Nikamnyati palikua ni mahali fulani kama korido ivi. Nikamfikia na kumbana vizuri kisha nikamnyonga bila kuchelewa. Kisha nikamlaza mle ndani nikaanza kutoka kurudi nje. Lakini wakati nageuka ili nipotee eneo lile nikasikia sauti ikisema kijana________________________

____________________________________________________________________________________________________________________________________Tukutane sehemu ya 32 tujue yaliyojiri huko jela. Nawapenda wote. Kwa lolote nicheki kwa mawasiliano hayo hapo juu.
Previous
Next Post »