HALI YA HEWA WAONYA UWAPO WA KIMBUNGA KITAKACHOSABABISHA MVUA KUBWA ANGALIA MIKOA ITAKAYOKUWA KATIKA HATARI YA KUKUBWA NA KIMBUNGA HICHO USIPUUZE

kimbunga_e3009.jpg
Machafuko ya hali ya hewa, mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetahadharisha juu ya kuwapo kwa kimbunga kiitwacho Hellen katika mwambao wa Bahari ya Hindi ambacho kitasababisha mvua kubwa inayozidi mililita 50 ndani ya saa 24 kuanzia jana katika mikoa 14. Taarifa ya mamlaka hiyo ambayo imetolewa jana kwa vyombo vya habari imebainisha kuwa mvua zitanyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtara, Lindi, Tanga, Unguja, Pemba, Singioda, Dodoma, Ruvuma, Katavi, Njombe, Mbeya na Morogoro. 
Pia Ripoti ya Umoja wa Mataifa imetahadharisha kwamba ongezeko la joto la dunia litakuwa na madhara mabaya zaidi na yasiyofidika. Wanasayansi na maafisa wa Umoja wa Mataifa wanaokutana nchini Japan wamesema kuwa, miongoni mwa madhara yatakayoikumba dunia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ni uwezekano mkubwa wa kutokea mafuriko, kuathiriwa mazao na ukosefu wa maji.
Ripoti hiyo iliyotolewa hii leo na Kamati ya Mataifa ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa imeonya kwamba, madhara ya ongezeko la joto la dunia huwenda yasiweze tena kudhibitiwa iwapo itashindikana kuzuia uchafuzi wa mazingira unatokana na gesi za nyumba ya kioo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, majanga yaliyoshuhudiwa katika karne ya 21 kama vile wimbi la joto kali barani Ulaya, moto uliokuteketeza misitu nchini Marekani, ukame huko Australia na mafuriko makubwa Msumbuji, Thailand na Pakistan yataongezeka duniani.
Previous
Next Post »