Duniani kuna
mambo, kuna vibweka na vibwakuro pia , twende sawa,Kang Hu, mwenye umri
wa miaka 33,aliwashtua wageni waalikwa siku ya harusi yake, pale
alipoamua kuwaomba radhi wakiwemo familia yake na bi harusi Na
Sung,mwenye umri wa miaka 30,kwa kumwambia dhahiri shahiri kuwa ana sura
mbaya na hafai kuolewa.
Bwana harusi harusi huyo alikanganyikiwa mara baada tu ya kumwona bi harusi wake kwa mara ya kwanza na kujaribu kujitosa majini.
Mara akaamua
kutoka eneo la tukio, kwenye ukumbi wa sherehe katika mji wa Shiyan mji
ulioko nchini China jimbo la Hubei na baadaye alioneka akitembea kando
ya mto akiwa na mawazo meeengi,mto ambao alijirusha ndaniye mara moja.
Pal Chan Wang
alisema kwamba : familia ya bi harusi ilivurugikiwa,familia ikashikwa na
ghadhabu,na familia ya mwanaume yao ikafura na marafiki zake
walifadhaika mnoo kwa matamshi yake .
Kang alikuwa na
uchaguzi wa bi harusi amtakaye na alikuwa akilazimishwa kumuoa bi
harusi huyo, ndo alipoamua kumfanyia kituko hicho.
Wapiti njia ndio waliomgundua Kang mtoni ndipo walipowaita polisi na kuharakisha kushuka mtoni kumuopoa.
Qan Tsui,
mwenye umri wa miaka25, yeye ndiye aliyepiga picha hizi anaeleza kwamba
bwana harusi huyo alipojitosa mtoni alikuwa na nguo zake zote na alikuwa
akielea uso ukiwa unaelekea chini kwenye maji,akiwa hajiwezi na mara
nikasema anaweza kufa asipopata msaada wa haraka.
polisi walipowasili eneo la tukio,mmoja wao alijitosa mtoni na kumdaka mara moja,na mwingine aliwarushia Kamba ili wamvutie nje ya maji ya mto huo baadaye wamtoe maji yaliyoko kifuani.
EmoticonEmoticon