Mbunge
wa jimbo la Makete Dkt Binilith Mahenge akiwa katika ziara yake katika
kijiji cha Kisasatu kata ya Mbalatse wilayani Makete
Na Eddy Blog
Suala
la wanafunzi wa shule ye sekondari Mbalatse kulala chini kutokana na
ukosefu wa vitanda katika bweni la wanafunzi shuleni hapo limeonekana
kuwa miongoni mwa kero sugu inayowaumiza kichwa wananchi wa kijiji cha
Mbalatse kata ya Mbalatese wilayani Makete mkoani Njombe
Hayo
yamebainika kwenye mkutano wa hadhara kati ya wananchi hao na mbunge wa
jimbo la Makete ambaye pia ni waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais
Mazingira Dkt. Binilith Mahenge uliofanyika katika kijiji hicho ambapo
pamoja na mbunge kueleza yaliyofanywa wakati wa uongozi wake lakini pia
alitoa fursa kwa wananchi kutoa waliyonayo
Pamoja
na kueleza kero mbalimbali zinazowakumba lakini hawakusita kusema jinsi
wamekuwa wakiumizwa na kitendo cha wanafunzi kulala chini kutokana na
ukosefu wa vitanda kwenye bweni la sekondari yao ya Mbalatse na kusema
wao kama wananchi wameshiriki kikamilifu katika ujenzi wa bweni hilo
isipokuwa wamekwama vitanda
Akijibu
hoja hiyo Mh Mahenge ameahidi kuleta vitanda vyote vya bweni hilo ili
kuondokana na kero hiyo na kusema kuwa hakuwa na taarifa za tatizo hilo
tangu awali kwa kuwa angelipatia ufumbuzi mapema iwezekanavyo
“Kwa
kweli niwe muwazi hapa, hili la watoto wetu wa sekondari kulala chini
limenigusa, na sijui ni kwa nini taarifa hizi hazijafikishwa kwangu
mapema na viongozi wa kata, lakini hata hivyo si mbaya naomba niahidi
hapa mbele yenu kwamba kuna wafadhili wamenipa msaada wa madawati 300 na
kwa awamu hii hapa wanatengeneza 100 nitawataarifu wapunguze kwenye
haya madawati 200 wanipe vitanda vyote vya hii sekondari, halafu na
madawati mengine yatakayobakia baada ya kutengeneza vitanda
Katika
hatua nyingine Dkt Mahenge amewataka viongozi mbalimbali wa kata hiyo
kutobaki kimya pindi wanapokumbana na changamoto, na badala yake wawe
wepesi wa kutoa taarifa maramoja kwa ngazi ya wilaya ambapo ni rahisi
kumfikia yeye ili atoe ushirikiano wake mapema katika kuzitatua kero
hizo na si kusubiri mpaka wananchi waje kuziibua kwenye mikutano
mbalimbali anayoifanya.
CREDIT TO EDDY BLOG
EmoticonEmoticon