TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 05.03.2015.







·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SABA KWA TUHUMA MBALIMBALI.

 
TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ELIZABETH SAIDURI (21) MKAZI WA IVUMWE ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA NOTI BANDIA MBILI ZA TSHS. 10,000/= ZIKIWA NA NAMBA AH 7889605 NA AG 4048159.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.03.2015 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA ENEO LA ILOMBA, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA AKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUNUNUA SIMU DUKANI.


KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KALANGALI WILAYANI CHUNYA AITWAYE HORO MASANJA (33) AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA LITA ISHIRINI (20).

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.03.2015 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA NKUNGU, KIJIJI CHA KALANGALI, KATA YA UPENDO, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.


KATIKA MSAKO WA TATU, MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA NKUNGU WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MILEMBE MAKELEMO (57) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA MICHE YA BHANGI 92 AKIWA AMEIPANDA KWENYE SHAMBA LAKE PAMOJA NA BHANGI YENYE UZITO WA KILO MBILI.


KATIKA MSAKO WA NNE, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SADIKI STEVEN (33) NA 2. MAWAZO STEVEN (29) WOTE WAKAZI WA IGANGWE WILAYANI CHUNYA WAKIWA WAMEPANDA BHANGI ENEO LENYE UKUBWA WA ROBO HEKA.

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.03.2015 MAJIRA YA SAA 14:15 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MASIMBA, KIJIJI CHA IGANGWE, KATA YA MTANILA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

KATIKA MSAKO WA TANO, MTU MMOJA MKAZI WA MANEGO WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KOMBE NDANI (29) AKIWA AMEPANDA MICHE YA BHANGI KWENYE  SHAMBA LENYE  UKUBWA WA ROBO HEKA.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.03.2015 MAJIRA YA SAA 14:15 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MANEGO, KIJIJI CHA MTANILA, KATA YA MTANILA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.


AIDHA KATIKA MSAKO WA SITA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KALANGALI WILAYANI CHUNYA AITWAYE ALLY MILAMBO (56) AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA LITA TATU [03].

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.03.2015 MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KONDE, KIJIJI CHA KALANGALI, KATA YA MTANILA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA WOTE WALIOKAMATWA KATIKA MATUKIO HAYO ZINAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI] NA POMBE YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA ULIMAJI WA BHANGI PAMOJA NA UPIKAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.



                                                  Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »