Basi
lililokuwa limebeba abiria waliokuwa wakitokea Mbeya kuelekea Dar es
salaam Lenye namba za usajili T438 CDE likiwa katika hali mbaya.
Watu 42 wamefariki maeneo ya Changalawe mji mdogo wa Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa baada ya basi la abiria lililokuwa likitokea mkoani Mbeya kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limetokea Dar es Salaam.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la
polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema tukio hilo limetokea
leo majira ya 09:30 asubuhi ikihusisha basi namba T:438 CDE likitokea
mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam na lori aina ya Scania namba T:689
APK lililokuwa
likiendeshwa na dereva Sebastiani Mgama likitokea Dar es Salaam kuelekea
Mbeya.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa kati ya watu 42 waliofariki
kwenye ajali hiyo wanaume ni 33,wanawake 6 na watoto 3 huku maiti nane
zimeshatambuliwa na ndugu zao na kuchukuliwa kwa ajili ya shughuli za mazishi.
Aidha amesema maiti hizo zilihifadhiwa kwa muda katika kituo kidogo cha afya cha
Mafinga na kisha kuhamishiwa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa pamoja na
majeruhi 22 wa ajali hiyo ambapo waliojeruhiwa kidogo wataendelea kupata
matibabu katika kituo cha afya cha mji mdogo wa Mafinga.
Kamanda Mungi amesema kuwa katika eneo hilo kuna bonde na
uchakavu wa barabara,kutokana na mwendo kasi wa dereva wa lori ambaye alikuwa
akijaribu kulikwepa shimo lililokuwa katikati ya barabara kabla ya kupishana na
basi la abiria.
Amesema kufuatia hali hiyo ikasababisha kupoteza mwelekeo kisha
kontena lililokuwa limebebwa na lori hilo kuliangukia basi la abiria ambalo kwa
muda huo lilikuwa karibu na lori hilo.
Hata hivo Kamanda Mungi amesema taarifa zaidi zitatolewa kesho Machi 12 ,2015 ambapo pia ametoa wito kwa wamiliki wa magari na
madereva kuwa makini wawapo barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama
barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
MAJINA YALIYOPATIKANA YA ABIRIA WALIOKUWA KATIKA BASI HILO HADI SASA NI: Baraka
Ndone (dereva), Yahya Hassan ( kondakta), Ester Emanuel, Lusekelo
Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni, Frank Chiwango, Luteni Sanga, Teresia
Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana,
Catherine Mwate, Mwajengo, Ndulile Kasambala, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala,
Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule
na Dominick Mashauri, Omega Mwakasege.
Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick
Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi,
Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa
Iman Mahenge , Juma Sindu, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule.
Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo
wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na
Oswald.
Basi hilo lilianza safari mjini Mbeya likiwa na abiria 37.
EmoticonEmoticon