MTU MMOJA MKAZI WA UHAMILA WILAYANI MBARALI AUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA KATIKA MFEREJI.



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 10.03.2015.

·         MTU MMOJA MKAZI WA UHAMILA WILAYANI MBARALI AUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA KATIKA MFEREJI.


·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SABA KWA MAKOSA MBALIMBALI.



KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA MKAZI WA UHAMILA WILAYANI MBARALI ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA REUS ELIAS AMOSI (50) ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA MWILI WAKE KUTUPWA KWENYE MFEREJI WA UMWAGILIAJI WA HIGHLAND ESTATE.

MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA KWENYE MFEREJI HUO MNAMO TAREHE 09.03.2015 MAJIRA YA SAA 12:45 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA UBARUKU, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA UKIWA UMEHARIBIKA.

INADAIWA KUWA KABLA YA TUKIO HILO MAREHEMU ALITOWEKA NYUMBANI TANGU TAREHE 24/02/2015 BAADA YA KUBAINIKA KUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA RUTH MSOSI (30) MKAZI WA ISISI AMBAYE MUME WAKE ALISHAFARIKI DUNIA SIKU NYINGI ZILIZOPITA  LAKINI ALIKUWA BADO ANAISHI KATIKA MJI WA MUME WAKE NA WATOTO.

KUTOKANA NA TUKIO HILO, WATU WANNE WAMEKAMATWA KWA MAHOJIANO AMBAO NI 1. RUTH MSOSI (30) 2. THOMAS MINZI (46) 3. STEFANO KIBWANA (50) NA 4. BELINA KIPAMANA (50) WOTE WAKAZI WA ISISI. MWILI WA MAREHEMU ULIFANYIWA UCHUNGUZI KISHA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI.


TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA UYOLE JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EDWARD COASTER (25) AKIWA NA KETE 80 ZA BHANGI ZENYE SAWA NA UZITO WA GRAM 400.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIFANYIKA MNAMO TAREHE 09.03.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO MTAA WA UYOLE, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA THOMAS ASAFA (28) AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.

MHAMIAJI HUYO ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 09.03.2015 MAJIRA YA SAA 23:45 USIKU KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO MTAA WA UYOLE, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.


KATIKA MSAKO WA TATU, WATU WAWILI WAKAZI WA AIRPORT JIJI MBEYA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. JULIUS STEVEN (27) NA 2. BENSON JACOB (25) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA KETE 03 ZA BHANGI ZENYE SAWA NA UZITO WA GRAM 15.

WATUHUMIWA KWA PAMOJA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 09.03.2015 MAJIRA YA SAA 17:50 JIONI HUKO MTAA WA AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.


AIDHA KATIKA MSAKO WA NNE, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. MICHO MWAKYUSA (27) MKAZI WA AIRPORT 2. RICHARD  MGAWE (35) MKAZI WA NZOVWE NA 3. JACKSON SABAKIA (42) MKAZI WA MBALIZI WAKIWA WANAKUNYWA POMBE KABLA YA MUDA.

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 09.03.2015 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO MWANJELWA, KATA YA LUANDA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTII SHERIA BILA SHURUTI ILI KUJIEPUSHA NA MATATIZO AU MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »