TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS
RELEASE” TAREHE 09.03.2015.
·
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA UTURO WILAYANI
MBARALI AMEKUTWA AMEUAWA NA KISHA KUNYOFOLEWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI.
·
MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA AFARIKI DUNIA
PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MOMBA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU SABA WAKIWA NA POMBE YA MOSHI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI
WA UTURO WILAYANI MBARALI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHARLES SIJAONA @ MATEMLA (55)
ALIKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI
SEHEMU ZA KICHWANI NA SHINGONI. AIDHA MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UKIWA
UMENYOFOLEWA SEHEMU ZA SIRI NA WATU HAO.
MWILI WA
MAREHEMU ULIKUTWA NJE YA NYUMBA ALIYOKUWA AKIISHI MNAMO TAREHE 08.03.2015 MAJIRA YA SAA
01:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA UTURO, KATA YA MAPOGOLO, TARAFA YA
ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA
MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO
HILO ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA MSAKO/UPELELEZI WA
KUWABAINI WALIHUSIKA KATIKA TUKIO HILI UNAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAFUNZI WA
DARASA LA KWANZA KATIKA SHULE YA MSINGI CHIPAKA ILIYOPO WILYANI MOMBA KATIKA
KIJIJI CHA NKANGAMO ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ENES DADISON (08)
ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.288
BCH AINA YA TOYOTA CRESTA
LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.03.2015
MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO
KATIKA KIJIJI NA KATA YA NKANGAMO, TARAFA YA TUNDUMA, KATIKA BARABARA YA
TUNDUMA/SUMBAWANGA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI
NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO. JITIHADA ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA. AIDHA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
SERIKALI TUNDUMA.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SABA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ESTER MWAKALINDILE (33) MKAZI WA
NDOLA 2. AYUBU MWANZYELE (28) MKAZI
WA MAPELELE 3. JOHN EMMANUEL (40)
MKAZI WA NDOLA 4. SAMWEL MWAKALINGA (30)
MKAZI WA NDOLA 5. ISSAMBI MWALYEGO (48)
MKAZI WA DDC 6. WEMA AMBAKISYE (32)
MKAZI WA NDOLA NA 7. ANGOLUISYE MWAMBAPA
(26) MKAZI WA NDOLA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO.
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE
08.03.2015 MAJIRA YA SAA 14:00
MCHANA HUKO MAENEO YA NDOLA KILABUNI, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA BONDE LA
USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
WATUHUMIWA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
KUFANIKISHA KUKAMATWA KWA DEREVA ALIYEHUSIKA KATIKA TUKIO AJALI AZITOE KWA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. AIDHA
ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE YA MOSHI KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon