WATU WATATU WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI KUBWA LA MIZIGO KUGONGA MAGARI MENGINE MATATU ENEO LA MLIMA MBALIZI.



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 23.02.2015.


·         WATU WATATU WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI KUBWA LA MIZIGO KUGONGA MAGARI MENGINE MATATU ENEO LA MLIMA MBALIZI.


·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU RAIA WA KONGO WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.

·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA SILAHA BUNDUKI KINYUME CHA SHERIA.
 
·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAKAZI WAWILI WA MPEMBA WILAYA YA MOMBA WAKIWA NA MICHE 10 YA BHANGI.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:

WATU WATATU KATI YAO MWANAUME MMOJA UMRI KATI YA MIAKA 45 – 50, MWANAMKE MMOJA UMRI KATI YA MIAKA 65 – 70 NA MTOTO WA KIKE UMRI KATI YA MIAKA 10 – 12 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.144 CGX/T.569 CKC AINA YA FAW TRACK LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA KUYAGONGA MAGARI MATATU AMBAYO NI T.158 BSJ AINA YA TOYOTA PICK-UP LIKIENDESHWA NA EMANUEL SHEDAFA (28) MKAZI WA MWAKIBETE, GARI T.584 DRB AINA YA TOYOTA HIACE LIKIENDESHWA NA DENIS VICTOR (27) MKAZI WA NZOVWE NA GARI T.623 ADQ AINA YA TOYOTA HIACE LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA AMBALO LILIPOTEZA UELEKEO NA KUTUMBUKIA MTONI NA KUSABABISHA VIFO.

AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 22.02.2015 MAJIRA YA SAA 16:45 JIONI HUKO ENEO LA MLIMA MBALIZI, KATA YA SONGWE, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU 14 WALIJERUHIWA KATI YAO 13 WAMELAZWA HOSPITALI TEULE YA IFISI NA MMOJA AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.

KATI YA MAJERUHI HAO 04 NI WANAWAKE NA 10 NI WANAUME. CHANZO CHA AJALI BADO HAKIJAFAHAMIKA. DEREVA WA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. NA T.144 CGX/T.569 CKC AINA YA FAW TRACK ALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.



TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SIFA BUKULU (35) NA 2. NYOTA RAMADHANI (30) PAMOJA NA WATOTO WADOGO WATATU WOTE RAIA NA WAKAZI WA SANGE NCHINI KONGO WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.

WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 22.02.2015 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO ENEO LA MAJENGO, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.










KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. AMANI MBEGA (43) MKAZI WA MOSHI NA 2. HAKIMU WATSON (40) MKAZI WA MAJENGO WAKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA SHOTGUN ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI NA RISASI MOJA.

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 22.02.2015 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITUMBA, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO. SILAHA HIYO ILIKUWA IMEFICHWA KWENYE DARI LA NYUMBA YAO.

KATIKA MSAKO WA TATU, WATU WAWILI WOTE WAKAZI WA MPEMBA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. LUCAS KAYUNI (28) NA 2. MANENO KAYUNI (20) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA MICHE 10 YA BHANGI IKIWA IMEPANDWA KWENYE SHAMBA.

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 22.02.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MPEMBA, KATA YA CHIWEZI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII WANANCHI NA KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA ALIKIMBIA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Previous
Next Post »