MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA MEZ B AFARIKI DUNIA LEO

 

Mwana Chemba MEZ B Afariki Dunia..
Mwanamuziki Moses Bushangama maarufu kama Mez B amefariki dunia leo saa nne asubuhi akiwa hospitali mjini Dodoma.

Imeelezwa kuwa Mez B ambaye alikuwa mmoja wa wasanii wanaounda kundi la Chamber Squard amefariki kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu yaani TB.

Umauti umemfika akiwa kwenye hospitali ya Mwananchi iliyopo mjini Dodoma alipokuwa akipata matibabu huku habari juu ya kifo chake zikithibitishwa na mama yake mzazi.

Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu marehemu Mez B ni kama ule wa Kama Vipi aliomshirikisha Mh. Temba na Nimekubali aliowashirikisha Ray C na Mwana Chemba mwenzake Noorah a.k.a Baba Style...

Pumzika kwa Amani MEZ B..
Previous
Next Post »