JK afanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya huku wengine wakitenguliwa

 
 Jakaya-Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  amefanya mabadiliko ya wakuu wa Wilaya ili kuboresha utendaji kazi. Mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi wazi ishiri na saba (27) zilizotokana na:
a) Kufariki dunia Wakuu wa Wilaya 3; b)Kupandishwa cheo Wakuu wa Wilaya 5 kuwa wakuu wa Wakuu wa Mikoa: c)Kupangiwa Majukumu Mengine wakuu wa Wilaya 7; na d)Kutengua uteuzi wa Wakuu Wawilaya wengine 12.
katika babadiliko hayo Rais Kikwete amewateua wakuu wapya wa Wilaya 27 kujaza nafasi hizo zilizo achwa wazi.
Aidha, Wakuu wa Wilaya sitini na nne (64) wamebadilishwa vituo vyao vya kazi na Wakuu wa Wilaya arobaini na mbili (42) wameendelea kubaki katika vituo vyao vya sasa. 
Walio teuliwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Zamani wa TFF, Freddrick Mwakalebela, Mtangazaji wa TBC, Shaban Kisu, Katibu wa Hamasa wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mboni Mhita na aliyewahi kuwa RPC, Zolothe Steven.



Walioacha ni pamoja na Elias Wawa Lali (ngorongoro), Alfred E. Msovella (Kiteto)Dk. Leticia M. Warioba (Iringa), James K. O. Millya (Longido), Mathew S. Sedoyeka (Sumbawanga),  Fatuma L. Kimario (Igunga),  Elias W. Lali (Ngorongoro), Abihudi M. Saideya, (Momba),Mrisho Gambo (Korogwe). 

Majina hayo yametangazwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mjini Dodoma mchana huu.
Previous
Next Post »