Mchungaji wa kanisa la Spiritual Church Of God Osia Mdolo
Na Saimeni Mgalula ,Momba -Mbeya
WACHUNGAJI na wananchi kwa ujumla wametakiwa kuliombe amani taifa
letu ili Tanzania ibaki kuwa nchi ya amani na sio ya vita hasa huu
mwaka wa nchi yetu kuwa na kazi kubwa ya undwaji wa katiba Mpya pamoja
na uchaguzi mkuu wa Kumpata Raisi , Wabunge pamoja na Madiwani.
Hayo yamesemwa na Mchungaji wa kanisa la Spiritual Church Of God Osia
Mdolo akilihubilia taifa kubaki na amani kama ilivyo zoeleka na
watanzania wengi, iliyofanyika katika kanisa hilo lililopo maeneo ya
kaloleni mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya.
Alisema kuwa nchi yetu ina kazi kubwa saana hasa kazi mbili za wananci
kuipigia kura Katiba inayo pendekezwa na uchaguzi mkuu ambao
unatarajiwa kufanyika mnamo Oktoba 30 mwaka huu ambapo bila amani ya
bwana taifa letu litachafuka.
‘’Wachungaji wote nwaomba waendelee kuiombea nchi yetu ili tuendelee
kuwa na maisha tulioyazoeya kuwa wana wa baba na mama mmoja bila ya
kuwa na ubaguzi wa kidini, rangi wala kabira maana tunajionea nchi za
wenzetu wanao shindwa kufikia mwafaka na kukubali matokeo ya
uchaguzi’’ alisema Pastor Mdolo.
Alisema kuwa kuna makanisa(Wachungaji} sasa yanaongelea siasa tu na
kuichanga na neno laMungu Madhabahuni ni makosa makubwa saana maana
madhabahuni ni mahali pa neno la Mungu na sio siasa.
‘’Huu ni wakakati wa kumuomba Mungu usiku na mchana iili aweze kutupa
katika iliyo bora itakayo tubadilisha wananchi kutoka maisha tunayo
ishi na kuwa bora aidi na sio katiba ya kuumlinda mtu mmoja ili aweze
kunemeka na rasilimali za watanzania’’ alisema.
Alisema kuwa ukihuzulia katika ibada nyingi za makanisa ya Kikristo
utakuta yanayoongelewa ni neno lillo jaa siasa ndani yake na huku
wengine wakitabili hata Raisi ajaye mala baada ya raisi wa awamu ya
nne Dr. Jakaya Kikwete mala baada ya muhula wake kumalizika.
‘’Hayo ni makosa na ni kumkufulu Mungu mana Mwanadamu huwezi kuingilia
kazi ya Mungu, hakuna mtu yeyote amjua raisi wa awamu ya tano hapa
nchi bali ni Mungu ppekee’’ alisema Mdolo.
Hata hivyo aliwataka viongozi kuwa na busala na kuamini matokeo
yatakayo tolewa pindi utakapo fika muda wa kuipigia kula katiba
inayopendekezwa nakuwa katiba ya kutuongoza watanzania wote na sio
baadhi ya wananchi (Viongozi).
‘’watanzania kwa sasa nadhani wanauchungu kuiona katiba mpya
inapatikana maana kila unapopita mtaani maada kuu ni kuhusiana na
upatukanaji wa Katiba Mpya na Uchaguzi mkuu wa kuwatafuta Madiwani ,
Wabunge na Raisi’’ alisema.
Alisema kama watanzania wote tunania ya dhati na taifa letu ili liwe
ni tmiongoni mwa mataifa makubwa na yenye amani hatuna budi ya
kushiliki kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kula na
kujitokeza kwa wingi katika kuipigia kula katiba mpya kushiliki kupiga
kula katika kuwatafuta viongozi watakao liongoza taifa hili wenye
busala na hekima na sio Mafisadi’’ alisema Mdolo.
EmoticonEmoticon