Na Saimeni Mgalula,Mbeya
Afisa forodha Mfawidhi wa (TRA) Raymond Mwanisawa wa kituo
kidogo cha Tunduma kilichopo Wilaya ya Momba,Mkoani hapa,amewapongeza baadhi wa
wafanyabashara kwakuanza kuwa waelewa katika swala la ulipaji wa kodi
serikalini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana ofisini
kwake,alisema kuwa,walio wengi walikuwa wanakwepakulipa kodi,kwasababu ya
kutokujua kwamba ulipaji wa kodi ni wajibu wao,kwani walichokuwa wanajua ni
kwamba mapato hayo wanakula viongozi wa TRA,alisema Raymond
‘’alisema kuwa,lakini
kutokana na kutoa elimu kwa wafanya biashara mara kwa mara kumepelekea baadhi yao kutokuwa
wabishi,alitoa mfano kuwa mnakuta mfanyabiashara anakwepa kulipa kodi kumbe
bidhaa zake hazitakiwi kulipia kodi alisema alisema Raymond.
Vilevile alifafanua juu ya watu ambao wanakwepa kodi na
kupitisha mizigo yao kwa njia za panya bila ya kulipia faini yake kwa gari ni
dora Elfu tano (5000) kwa gari bado mzigo ambayo nayo huifanyia Tathimini yake
ya kuiripia.
Pia alitoa ushauri kwa wafanyabiasha kwa mwaka huu
mpya,alisema kuwa wafanya biashara wafahamu kwamba kulipa kodi ni kwaajili ya
umma na pesa hizo hizo ndio zinazotumik a kutengenezea barabara kama barabara
ya Mpanda mpaka sumbawanga ni TRA NA Tunduma mpka mpanda ni kwa hisani ya watu
wa Marekani alisema Raymond.
‘’Aliendelea kwa kusema kuwa wasibebe didhaa bila kulipia
ushuru na alitoa ufafanuzi wa baadhi ya bidhaa ambazo hawalipii ushuru alisema
mfano Tackita halina ushuru ila vifaa vyake ndo vinatolewa ushuru alisema hivyo
Raymond
N a kwa upande wa baadhi ya wafanya biashara ambao majina
yao hawakupenda yaandikwe kwenye gazeti walisema kuwa hata sisi inatakiwa
tubadilike ili kuepuka kusumbuliwa na TRA kwani mtu ukilipia mzigo na kibali ukiwa
nacho hawatakusumbua waliema wafanya biashara hao .
Pia waliwataka Wafanya biashara wenzao kuwa,wawe wepesi wa
kulipa kodi ili kuepuka usumbufu kwasasabu unakwepa alafu,ukija kushikwa
unakuja kulipa mara nne yake,sasa hapo unakuwa umefanya nini walisema hivyo.
Na mwisho walimalizia kwa kusema kuwa wafanya biashara tulio
wengi hatuja soma kwahiyo wameiomba serikali kutoa elimu zaidi juu ya ulipaji
wa kodi kwa wafanya biashara ili wawe na uelewa juu ya maswala hayo na sio
kukwepa walimalizia hivyo.
EmoticonEmoticon