TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 19.01.2015.





DEREVA AFARIKI DUNIA BAADA YA GARI ALILOKUWA AKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA WILAYANI MBOZI.


DEREVA ALIYEKUWA AKIENDESHA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.910 CVF AINA YA TOYOTA NOAH ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA STANFORD LUENJE (30) MKAZI WA MBOZI ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI HILO KUACHA NJIA NA KUPINDUKA HUKO ENEO LA MLOWO WILAYANI MBOZI.

TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01:30 HUKO ENEO LA MLOWO, KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.

AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA  1. NDIMYAKE MWAKISU (33) NA 2. ELISHA MWASHUYA (30) WOTE WAKAZI WA MBOZI WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI KWA MATIBABU. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

Imesainiwa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »