Majambazi Wavamia Polisi, Wauwa Askari na Kuiba Silaha



Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzani, IGP, Ernest Mangu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzani, IGP, Ernest Mangu.

MAJAMBAZI wasiojulikana idadi yao usiku wa kuamkia leo wamevamia Kituo cha Polisi Ikwiriri Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani na kuwauwa askari polisi wawili pamoja na kupora silaha adhaa zilizokuwa zimehifadhiwa kituoni hapo.

Taarifa zilizotufikia kutoka eneo la tukio zinasema majambazi hao wasiojulikana idadi yao wakiwa na silaha mbalimbali majira ya saa nane kasorobo za usiku wa kuamkia leo walivamia katika kituo hicho na kuwauwa askari E.8732 CPL EDGER MILINGA pamoja na WP 5558 PC JUDITH TIMOTH kabla ya kufanya uporaji huo.

Taarifa za awali zinasema majambazi hao wanadaiwa kupora silaha saba SMG 2, SAR 3, Silaha ya mabomu ya machozi na silaha moja aina ya Short Gun mali ya kampuni ya Sigara TTCL. Taarifa zinasema kuwa majambazi hao pia wameharibu gari moja la polisi PT 1965 kwa risasi. Mtandao huu unaendelea kufuatilia taarifa zaidi zitakapo tufikia tutawajuza.
Previous
Next Post »