TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS
RELEASE” TAREHE 22.01.2015.
·
MTOTO WA MIAKA 04 AMEKUFA MAJI KATIKA MTO SAZA
WILAYANI CHUNYA WAKATI AKIVUKA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI WAKIWA NA MALI ZINAZODHANIWA KUWA NI ZA WIZI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTOTO MWENYE
UMRI WA MIAKA 04 ALIYETAMBULIKA KWA
JINA LA MIRAJI ATHUMANI MKAZI WA
MALEZA WILAYANI CHUNYA AMEKUFA MAJI BAADA YA KUTUMBUKIA KATIKA MTO SAZA WAKATI
AKIVUKA KWENDA NG’AMBO YA PILI YA MTO HUO.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 21.01.2015
MAJIRA YA SAA 07:33 ASUBUHI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA SAZA FALLS, KIJIJI CHA MALEZA, KATA YA MBANGA, TARAFA YA
KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA
CHANZO CHA KIFO HICHO NI BAADA YA MAREHEMU KUMTOROKA BIBI YAKE AITWAYE ELIZABETH HANGO (62) MKAZI WA MALEZA NA
KUMFUATA MAMA YAKE AITWAYE LATIFA GOSKA
(25) MKAZI WA SAZA FALLS ALIYEKUWA SHAMBANI NG’AMBO YA MTO HUO AKIENDELEA
NA KILIMO NA NDIPO MTOTO HUYO ALITEREZA NA KUTUMBUKIA KATIKA MTO HUO NA KUPELEKEA
KIFO CHAKE. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA
MAZISHI.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA
WATOTO WAO IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA HASA KATIKA KIPINDI
HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. YOHANA
JACKSON (45) MKAZI WA IGANZO NA 2.
JUMANNE MWINGINE (48) MKAZI WA UYOLE
WAKIWA NA MITA 19 ZA MAJI MALI YA
IDARA YA MAJI MBEYA ZINAZODHANIWA KUWA NI ZA WIZI.
WATUHUMIWA HAO
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 21.01.2015
MAJIRA YA SAA 16:45 JIONI HUKO
KATIKA MTAA WA JUHUDI, KATA YA ILEMI, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
MITA HIZO ZILIKUTWA NYUMBANI KWA MTUHUMIWA NAMBA 1 YOHANA JACKSON MARA BAADA YA KUFANYA UPEKUZI. TARATIBU ZA
KUWASILIANA NA IDARA YA MAJI MBEYA KWA UCHUNGUZI ZAIDI NA UTAMBUZI WA MITA HIZO
UNAENDELEA.
Imesainiwa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon