Lori
maalumu la usafishaji likiondoa theluji iliyoenea katika barabara ya
South Church Street, katika mji wa Hazleton, Pennsylvania siku ya
Jumatatu Jan 26, 2015. Photo via .dailymail.co.uk
By Abou Shatry Washington DC
Zaidi
ya watu 60 million wataathirika kutokana na kimbunga kikubwa cha upepo
unaoambatana na unyeshaji wa theleji katika eneo la kaskazini mashariki
ya Marekani.
Kwa
mujibu wa kitengo cha hali ya hewa nchini Marekani, imetaja maeneo
ambayo yataathiriwa na dhoruba hiyo, ya kihistoria ambayo itapelekea
zaidi ya watu kadhaa kukosa huduma ya umeme, pamoja na huduma za usafiri
wa anga na nchi kavu.
Imetaja
baadhi ya majimbo ambayo yatakumbwa na kimbunga hicho kuwa ni New York,
New Jersey, Massachusetts, Connecticut na Rhode Island, ambapo viongozi
wakuu wamajimbo hayo kutangaza hali ya hatari kwa tukio hilo ambalo
litatokea siku ya Jumatatu, Jumanne na Jumatano.
Imetabiriwa
kiasi cha unyeshaji wa theluji hiyo 36inches katika jimbo la New York
16 hadi 26 inches katika jimbo la Boston, na kiwango chengine kama hicho
katika baadhi ya majimbo mengine.
Zaidi
ya safari za ndege 3,800 zimesimamishwa mapema leo katika viwavya vya
ndege vya JFK, LaGuardia na Newark airports, pia huduma za shule
kufungwa siku ya jumanne na jumatano katika majimbo hayo.
EmoticonEmoticon