TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 11.12.2014.






·         MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI.




·         MTU MMOJA MWENYE ASILI YA KISOMALI/KIETHIOPIA AMEKUTWA AMEKUFA VICHAKANI WILAYANI MBOZI.




·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU WANNE RAIA WA NCHINI KONGO.





·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAKAMATA POMBE HARAMU YA MOSHI WILAYANI KYELA.






KATIKA TUKIO LA KWANZA:


MWENDESHA PIKIPIKI AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.547 CBP AINA YA FECON ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.779 BNE/T.266 BNH AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE HUSSEIN JUMA (22) MKAZI WA ARUSHA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 10.12.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO MAENEO YA KADEGE, KATA YA FOREST, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WATAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.



KATIKA TUKIO LA PILI:


MTU MMOJA MWENYE ASILI YA KISOMALI/KIETHIOPIA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA, JINSI YA KIUME, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 25-30 AMEKUTWA AMEKUFA VICHAKANI MITA TATU KUTOKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.

MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA ENEO LA KIJIJI CHA KILIMAMPIMBINI, KATA YA VWAWA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA MNAMO TAREHE 10.12.2014 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI. MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA UKIWA HAUNA JERAHA LOLOTE NA UKIWA UMEDHOOFIKA SANA.

AIDHA BAADA YA KUMPEKUA MFUKONI ALIKUTWA NA TIKETI YA BASI LA RATCO EXPRESS ILIYOKUWA NA JINA LA ELY FAMILY MDUNDO KUTOKA TANGA KWENDA DSM ILIYOKATWA TAREHE 04.11.2014 YA KUSAFIRI TAREHE 6.11.2014. INADHANIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA NI MHAMIAJI HARAMU. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA SERIKALI WILAYA YA MBOZI. UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.




TAARIFA ZA MISAKO:


KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WANNE WA NCHINI KONGO KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI. WAHAMIAJI HAO NI PAMOJA NA 1. HASSAN KAULA (18) 2. KATUMBA ASHERI (20) 3. ISSAH LUKIMBANA (20) NA 4. IBELE BUMA (20).

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 10.12.2014 MAJIRA YA SAA 13:20 MCHANA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA ENEO LA KASUMULU MPAKANI, KATA YA NGANA, TARAFA YA NTEMBELA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.


KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAKAMATA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 10 IKIWA KWENYE BAISKELI BAADA YA KUFANYIKA MSAKO MNAMO TAREHE 10.12.2014 MAJIRA YA SAA 11:30 ASUBUHI HUKO KATIKA ENEO LA NDANDALO, KATA YA KYELA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA KYELA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA KUWAONA ASKARI NA KUTELEKEZA POMBE HIYO NA BAISKELI. JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAGENI KUFUATA TARATIBU ZA KUINGIA NCHINI KIHALALI ILI KUEPUKA MATATIZO. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI/UPIKAJI WA POMBE YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »