Muongozaji
wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi, Jordan Riber akizungumza katika
uzinduzi wa tamthilia hiyo Sehemu ya pili kwenye ukumbi wa Cinemax
Century jijini Dar es salaam.
MC wa shughuli ya uzinduzi wa Siri ya Mtungi 2, Ambi Lusekelo akimtambulisha muigizaji nyota wa tamthilia hiyo, Cheche
Katibu Mtendaji
wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo Katikati na wadau wa
Filamu Tanzania waliohudhuria katika uzinduzi huo wakifuatikia hotuba
bali mbali zilizotolewa wakati wa uzinduzi wa Tamthilia ya Siri ya
Mtungi awamu ya pili.
Maofisa
kutoka kampuni ya John Hopkins University For Communication Programs
(JHU CCP) ambao moja wa wadhamini wa tamthilia hiyo katika picha ya
pamoja.
Le Mutuz
akiwa na mmoja wa waigizaji wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi awamu ya pili
Richa Adhia, Msemaji wa Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda na
Muigizaji mkongwe nchini, Mwita nao walikuwepo katika uzinduzi huo
Le Mutuz akiwa na Msemaji wa Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda
Waigizaji wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya uzinduzi rasmi kwenye ukumbi wa Cinemax Century
Na Mwandishi wetu
Bodi
ya Filamu Tanzania imewataka waandaaji wengine wa fani hiyo kuiga mfano
wa waandaaji wa tamthilia ya Siri ya Mtungi, Shirika Lisilo la
Kiserikali (NGO ya Media for Development International Tanzania
(MFDI-TZ) kwa kutoa filamu yenye mafundisho mbali ya kuburudisha.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce
Fissoo kupitia kwa mwakilishi wake, Beatrice Sumari kwenye ukumbi wa
Cinemax Century wakati wa uzinduzi rasmi uliowashirikisha wadau wa fani
hiyo, wadhamini na waandaaji.
Sumari
alisema kuwa Tamthilia ya Siri ya Mtungi Msimu wa Pili mbali ya
kuburudisha, pia imetoa ajira kwa Watanzania wengi, pia imeleta
changamoto kuhusiana na mabadiliko ya tabia kwa jamii.
“Filamu
imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, hii ni fursa kwa wadau wa fani
hiyo kuiga MFDI-Tanzania kwa kuleta katika jamii filamu yenye ubora huu,
naomba wengine wafuate nyayo zao,” alisema Sumari.
“Filamu
hiyo ina ubora wa picha, sauti, maudhui na mfuatano wa matukio wa
kipekee na kuleta burudani ya aina yake.. ni tamthilia ambayo ukianza
kuangalia, hauta kinai na kuwa na hamu ya kufuatilia kile kinachofuata,”
alisema.
Afisa
kutoka Taasisi ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Ana Bodipo
alisema kuwa wanajisikia furaha kudhamini tamthilia hiyo ambayo
imezungumzia maisha halisi ya Mtanzania.
Bodipo
alisema kuwa alisema kuwa tamthilia hiyo inaelekeza jamii kuhusiana na
ugonjwa hatari wa Ukimwi na kwa wao ni moja ya nyenzo ya kushiriki
katika masuala ya afya katika maeneo mbalimbali nchini.
“Matukio
mengi katika tamthilia hii yana akisi taswira ya kweli katika jamii na
na kuwafanya wafuatiliaji kupata somo halisi kutokana na changamoto
mbalimbali,” alisema Bodipo.
Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka taasisi ya Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) alisema kuwa wamefuraishwa na mapokeo ya tamthilia hiyo pamoja na kuhitimisha na kufichua kilichopo katika mtungini.
Alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza.
Kamin
alisema kuwa kukamilika kwa hatua ya pili kunatokana na udhamini mnono
wa the John Hopkins University Centre for Communication Programs (JHU
CCP) ambao walitoa uongozi wa elimu na mkakati katika tamthilia, taasisi
ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Wizara ya Afya Ustawi wa
Jamii na MFDI.
EmoticonEmoticon