TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 11.11.2014.






Ø  MTU MMOJA  ASIYEFAHAMIKA AFARIKI DUNIA  KUFUATIA AJALI YA MAGARI MAWILI  KUWAGONGANA  JIJINI MBEYA.


Ø  MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA BAADA YA KUKUTWA MAHUTUTI KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI.




Ø  JESHI LA POLISI LINAWASHILIA WATU 15 RAIA WA NCHINI BURUNDI  KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI WILAYA YA ILEJE.



Ø  JESHI LA POLISILINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KUKAMATWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] JIJINI MBEYA.


TUKIO LA KWANZA.


MTU MMOJA  ASIYEFAHAMIKA AFARIKI DUNIA  KUFUATIA AJALI YA MAGARI MAWILI  KUGONGANA.

MTU MMOJA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI,  ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO KATIKA AJALI YA MAGARI  MAWILI KUWAGONGA ENEO LA MBALIZI.

TUKIO HILO LIEMTOKEA TAREHE 10.11.2014 MAJIRA YA SAA 11:00HRS  KATIKA ENEO LA MBALIZI-KATA YA UTENGULE-USONGWE, TARAFA YA BONDE LA SONGWE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA  MBEYA, BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA, KUFUATIA AJALI ILIYOHUSISHA  MAGARI MAWILI  T.824 AUT/.T.935 AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA BRYSON  HANS [26], MKAZI WA KIMARA-DSM NA GARI T.420 ANZ AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA TROMEO MWIHIHOLA[52],MKAZI WA SONGWE KISHA KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU HUYO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.

 HATA HIVYO MARA BAADA YA AJALI DEREVA WA GARI T.420 ANZ ALIKIMBIA NA GARI LAKE NA DEREVA WA GARI T.834 ATK AMEKAMATWA   NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA  WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYEKIMBIA  AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.


TUKIO LA PILI


MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA BAADA YA KUKUTWA MAHUTUTI KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI.

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KASSIM RASHID [55],MKAZI WA GHANA – MBEYA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA RUFAA JIJINI MBEYA.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 10.11.2014 MAJIRA YA SAA 16:30HRS. AWALI MAJIRA YA SAA 09:30HRS MAREHEMU ALIFIKA KWENYE NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO ATUKUZWE ILIYOPO ENEO LA SOKOMATOLA AKIWA AMEONGOZANA NA MWANAMKE MMOJA AMBAYE HATA HIVYO HAKUWEZA KUFAHAMIKA MARA MOJA JINA NA MAKAZI YAKE NA KUCHUKUA CHUMBA NAMBA 6. BAADA YA DAKIKA 20,MWANAMKE HUYO ALITOKA CHUMBANI HUMO NA KWENDA KUSIKOJULIKANA. HATA HIVYO MAJIRA YA SAA 12:00HRS MHUDUMU WA NYUMBA HIYO YA KULALA WAGENI NICKSON KAHANGA [24] WAKATI ANAPITA KUELEKEA UANI ALISIKIA KELELE ZA MTU KUKOROMA KATIKA CHUMBA NAMBA 6 NA ALIPOFUNGUA ALIMKUTA MAREHEMU AKIWA AMEJIFUNIKA BLANKETI MWILI MZIMA AKIWA MAHUTUTI ANAKOROMA  HAJITAMBUI. AIDHA  TAARIFA ZILIFIKISHWA POLISI KATI NA MHANGA ALIKIMBIZWA HOSPITALI NA MUDA MFUPI BAADAE ALIFARIKI DUNIA.

UCHUNGUZI ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO UNAENDELEA. IKIWA NI PAMOJA NA KUUFANYIA UCHUNGUZI WA KITABIBU WA MWILI WA MAREHEMU.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA  WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MWANAMKE ALIYEKUWA NA MAREHEMU AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.


TAARIFA ZA MISAKO


JESHI LA POLISI LINAWASHILIA WATU 15 RAIA WA NCHINI BURUNDI  KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI WILAYA YA ILEJE.

 KATIKA TUKIO LA KWANZA JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA  WATU 15 RAI WA NCHINI BURUNDI KWA KOSA LA KUNGIA NCHINI BILA KIBALI KATI YAO WATU WAZIMA NI WATATU NA WATOTO 12 AMBAO NI PAMOJA NA 1. KWIZERA WILLIAM  [30], 2. LUCY ZINAHONA [30] 3. MUSSA LAMECK [19], 4. NKULUNZINZA ASENCHI[5], 5. FURAHA MISHELINI [4],6. FEDHAIMANA NAKILA [4], 7. MUGISHA KELEZOKE [5], 8. ZAWADI ANITA[5], 9. NEEMA ESELI [4] 10. NKULUZINZA SENKYA[5], 11. DEOSIA YAMUNGU [4. 12. EYAKUZYE IYANAHA [5], 13.YUKUSENDE ESENHE [5],14. ALAKAZA ELEKISYE [MIEZI 2] NA 15. MUKUZINA STANLEY [3].

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 10.11.2014 MAJIRA YA SAA 21:50HRS HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA ISONGOLE,TARAFA YA BULAMBYA, WILAYA YA ILEJE MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI.

JESHI LA POLISILINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KUKAMATWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] JIJINI MBEYA.


KATIKA TUKIO LA PILI  JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA  ESTER SEME  [28], MKAZI WA   AIRPORT, BAADA YA KUKAMATWA  AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA 2 ½ .

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 10.11.2014 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA SOKONI-MANGA,  KATA YA MANGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA  MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI  MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI  ANATOA  WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU, KIKUNDI AU MTANDAO WA WANAOJIHUSISHA NA USAFIRISHAJI WA BINADAMU HUSUSANI WAHAMIAJI HARAMU  AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZIWEZE KUCHUKULIWA MARA MOJA.AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


Imetolewa na :-
[ AHMED  Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »