Siku moja baada ya wabunge kupinga hatua ya kutaka kutumia Mhimili wa mahakama kuzuia mjadala wa sakata la akaunti ya tegeta Escrow bungeni, bunge limesema hakuna barua ya mahakama iliyolizuia kujadili jambo lolote likiwemo sakata la wizi wa fedha za tegeta Escrow.
Akitoa maelezo hayo bungeni, mwenyekiti wa kikao cha 14 cha
bunge,Mhe.Mussa Azzan Zungu amewataka wabunge kuacha kuzungumzia swala
la barua hiyo kwa kuwa hakuna barua yeyote ya mahakama iliyozuia na
mahusiano kati ya mihimili hiyo miwili itaendela kuwa mazuri.
Hatua hiyo ya mwenyekiti wa kikao hicho imekuja kufutia msemaji wa
kambi ya upinzani Mhe.Moses Machali kusema njama za kuzuia sakata la
Escrow kujadiliwa bungeni linalenga kuwalinda viongozi wa serikali na
taasisi zake waliohusika na wizi huo jambo ambalo ni hatari kwa
mustakali wa taifa.
Wakichangia azimio la bunge la kuridhia itifaki ya uzuiaji wa
vitendo haramu dhidi ya miundombinu ya kudumu iliyojengwa chini ya
bahari katika mwambao wa bara la afrika 1988,baadhi ya wabunge wamedai
kuharakishwa kuridhiwa kwa azimio hilo baada ya kutoletwa katika bunge
kwa zaidi ya miaka 26 ni kutokana na zoezi la utafutaji mafuta na gesi
jambo ambalo serikali ilitakiwa kuacha wazi.
Akifafanua hoja za baadhi ya wabunge baada ya kuwasilisha azimio
hilo,waziri wa uchukuzi Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe amesema nchi 140
zimeridhia azimio la kuridhia itifaki hiyo ambayo inalenga nchi
wanachama wa itifaki kuwa na mikakati ya pamoja ya kulinda usalama wa
miundombinu na maisha ya watu walioko kwenye miundombinu pamoja na
kuweka adhabu kulinda uhalifu.
EmoticonEmoticon