Licha ya baadhi ya wazee hao wachache kuonyesha hali ya kukata
tamaa kutokana na maradhi yanayowasumbua yakiwemo ya kupooza kwa viungo
huku wengine wakishindwa kutoka nje wamesema kwa takribani miezi sita
sasa wamekosa chakula cha uhakika ama mlo wanaoupata hauna kitoweo ama
mboga,huku wadudu hao pia wakiwanyima usingizi.
Kufuatia kuwepo kwa changamoto ya wazee hao ,Benki ya posta
imekimbiza msaada wa haraka wa chakula na matunda pamoja na vifaa vya
usafi,huku ,msimamizi wa kituo hicho cha Sarame Bw Samson munuo akikiri
kuwepo kwa changamoto hizo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wahudumu.
Akikabidhi msaada huo uliokwenda sambamba na sherehe za Eid el
hadji,meneja wa benki ya Posta tawi la babati Bw Charles Woiso amesema
baada ya kusikia uvumi wa changamoto hizo na kuwatembelea wazee hao
benki hiyo imelazimika kusaidia msaada huo ili kupunguza makali ya njaa
uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 1.5 pamoja na kufanya usafi
katika eneo hilo.
EmoticonEmoticon